Kilichouzwa nje ni Madini, Sio mchanga
"Biashara ya uuzwaji wa Makinikia
haikufanyika kwa ushindani na si kweli kwamba wanauza Makinikia,
kinachouzwa ni madini." amesema Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza
mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro
Prof. Osoro ameyasema hayo wakati akikabidhi ripoti ya kamati yake kwa
Rais John Magufuli leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa gharama za shughuli za utafutaji na upembuzi madini nchini
zimejumuishwa katika mauzo yake kwa kupunguza faida hivyo hawatozwi
kodi.
"Faida yote iliyopatikana katika uuzwaji wa dhahabu nje haikujumuishwa
katika mahesabu ili kukwepa malipo ya mrabaha" alisema Prof. Osoro
Ameongeza kuwa uchunguzi wa kamati yake umebaini kuwepo kwa
utakatishwaji haramu wa fedha na faida kurudishwa kama mkopo kwa
makampuni ya madini kitu ambacho ni kinyume cha taratibu.
Comments
Post a Comment