MO AKUBALI KUISAIDIA SIMBA MILLIONI 200
Wachezaji
muhimu wanataka kusepa Simba baada ya mikataba yao Kuisha Simba
walimshirikisha tajiri Mohamed Dewji Kwa Ajili ya kuwasaidia kuwabakiza
wachezaji hao mhimu.
Kutokana
na ripoti ya kocha wa Simba ameshauri waongezwe wachezaji sita wa kazi
golikipa mmoja, beki watatu, Winga mmoja, na Mshambuliaji mmoja, Katika
ripoti hiyo inatabainisha kuwa wachezaji ambao hawajaisaidia timu hata
kwa asilimia 20 waachwe hata kwa kupelekwa Kwa mkopo. Pia ripoti
ikasisitizia wachezaji mhimu wasiondoke kwenye timu kama mikataba
imeisha waongezewe.
Baada
ya ripoti hiyo kukabidhiwa kamati ya utendaji ya kupelekwa Kwa kamati
ya usajili chini ya Zacharia Hanspope ikajadiliwa na ikaonekana
Mapendekezo ya Omog yatafuatwa Kwa asilimia zote tatizo likaja Kwa
wachezaji mhimu ambao wanamaliza mikataba ikawa changamoto kubwa. Ndio
kamati ikapeleka barua ya ombi Kwa tajiri kijana MO aweze kuwasaidia.
Baada
ya Mo kupokea barua hiyo aliwakubalia Simba Kwa Sharti moja tu fedha
ambayo ataitoa iwekwe kwenye mchakato wa mabadiliko ya Simba. Mjumbe
mmoja kutoka kamati ya usajili ambaye ni rafiki wa Mo ameagizwa
kuzungumza na wachezaji wanne (Mkude, Ajibu, Kotei na Banda) ili kuona
namna ambavyo wanaweza kubaki katika tetesi za usajili Mkude anataka
milion 70 na kuendelea, Ajibu anataka Milioni 50, Banda na Kotei wote
wanataka milioni 40 kila mmoja mambo yakienda Sawa MO atatoa milioni 200
kuwabakiza Nyota hao.
Mpaka
sasa Simba imetumia zaidi ya Milioni 200 kuwasajili Nyota watano watatu
kutoka azam (Manula, Kapombe, Bocco) Jamali Mwambeleko kutoka Mbao na
Yusuph Mlipili kutoka Toto . Ikiwa Manula Milioni 70, Kapombe milioni
50, Bocco milioni 47, Mwambeleko milioni 30, na Mlipili milioni 10 .
Comments
Post a Comment