MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE YATOKANAYO NA IMANI ZA KISHIRIKINA WILAYANI MAGU.



TAREHE 13.06.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA KISABO KATA YA BUJASHI TARAFA YA SANJO WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, NUNGHU MGETA, MIAKA 35, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KISABO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE AITWAYE MISUNGWI NUNGHU MIAKA 06, MTOTO WA KIUME, AMBAPO INADAIWA KUWA ALIMUUA KWA KUMZIBA MDOMO NA PUA KWA MUDA MREFU HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUSHINDWA KUPUMUA NA BADAE KKUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE MWENYEWE HAPO NYUMBANI KWAKE, KWANI TAYARI ALIKUWA AMETENGANA NA MKEWE KWA MUDA MREFU. INADAIWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUTELEKEZA MAUAJI HAYO ALIMCHUKUA MAREHEMU KISHA KWENDA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI LILILOPO MBALI NA NYUMBA YAKE ILI IONEKANE AMEKUFA MAJI.

ASUBUHI WAKATI WANANCHI WANAPITA MAENEO HAYO NA KUONA MWILI WA MTOTO ALIYEPOTEZA MAISHA UKIELEA KWENYE MAJI WALIPATA MASHAKA KISHA WALITOA TAARIFA KWENYE KITUO CHA POLISI, ASKARI BAADA YA KUPATA TAARIFA WALIFANYA UFATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA.

AIDHA KATIKA UCHUNGUZI WA AWALI MTUHUMIWA AMEKIRI KUTEKELEZA MAUAJI HAYO DHIDI YA MTOTO WAKE YANATOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA ILI APATE UTAJIRI. POLISI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWAMBA HAKUNA MTU YEYETO ALIYE JUU YA SHERIA HIVYO KILA MTU AHESHIMU NA KUULINDA UTU WA MWINGINE, LAKINI PIA ANATAKA WANANCHI WAFANYE KAZI ZILIZO HALALI ZA KUWAPATIA KIPATO NA KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA NA UHALIFU ILI WASIJE KUINGIA KWENYE MATATIZO.

IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Comments

Popular posts from this blog