MTOTO WA MIAKA 12, MOHAMED ABDULLAH AIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN BARANI AFRIKA
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa
Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa
mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu) MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed
Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000
(sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya
kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.
Mohammed
ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote
(mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta
iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo
kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Juni 11, 2017), Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo ni Taasisi ya
Al-Hikma waangalie uwezekano wa kuboresha zawadi kwa kutoa scholarships
(udhamini) kwa washindi au washiriki, hususan kwa washiriki wa
Tanzania.
“Ongeeni
na nchi marafiki kama Saudi Arabia, waone uwezekano wa kutoa zawadi za
ufadhili kwenye masomo ya sekta za kimkakati kama vile mafuta na gesi,
ili kuongeza hamasa na chachu ya vijana walioko kwenye sekondari zetu
nao waone fursa hii na kuichangamkia, badala ya mashindano kujikita
kwenye madrasa peke yake,” amesema. Waziri Mkuu amewataka wazazi
wafuatilie nyendo za vijana wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa
za kulevya na vitendo vingine viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao
na ustawi wa nchi yetu lakini akasisitiza pia waisaidie Serikali katika
mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi.
Waziri
Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11
ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017.
Waziri
Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya
Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa
Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa
mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mlezi wa Taasisi ya Al- Hikma Foundation,
Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 18
ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakar Zubeir bin Ally (kulia) na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed
Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na
Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo , katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya
Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Sharif Abduqadir
Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikma
Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo, katika Mashindano ya 18 ya
Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Comments
Post a Comment