KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI ACACIA ILIINGIA KINYEMELA NA HAINA KIBALI CHOCHOTE
Taarifa
ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo
kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Joseph
Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na
inafanya kazi kinyume cha sheria.Prof. Osoro amesema kwamba Kamati yake
imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini
na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu
uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.Aidha Kamati ya Prof. Osoro
imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia
hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba katika
mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya
mikataba hiyo.Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo
serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili
ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07,
mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini
kwenye makontena yote 44,277 tangu mwaka 1998 ni Tsh. tril 132.56.Pamoja
na hayo imebainika kuwa uongezwaji wa leseni kinyume cha sheria ambapo
imedaiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na
Sospeter Muhongo ndio waliohusika na uongezaji wa muda kwenye uchimbaji
wa madini.
Kamati
hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kuchukua sheria juu ya
kampuni ya ACACIA iliyopo nchini kinyume cha sheria kupitia msajili wa
makampuni ikiwa ni pamoja na Mawaziri wote walioshiriki kwa namna moja
au nyingine juu ya mikataba ya uchimbaji madini huku ikiitaka Serikali
iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye makampuni ya madini.
Comments
Post a Comment