Alichosema Zitto Kabwe baada ya ripoti ya madini
"Mwisho wa siku historia inaandikwa tu. Uzalendo ni kufanya jambo ambalo
wengi hawakuelewi lakini wewe unajua Ni jambo sahihi na unakubali
kutukanwa, kususubikwa, kusimangwa, kuzushiwa, nk. Unapambana tu. Mwisho
wa siku waliokuita msaliti watakuita shujaa. Waliokuzomea
wanashangilia. Wewe unafanya nini? Unakaa kimya kwani kwenye kukaa kimya
pia kuna kusema kukubwa zaidi. Muhimu Nchi ifaidike.
Huko nyuma nilipata kusema, hata mungu akinichukua sasa unakwenda ukiwa
umetabasamu kwani unakuwa umetimiza wajibu wako duniani. Kina Josina Umm
Kulthum wataishi Kwa heshima inshallah" Ameandika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook mara baada ya ripoti ya pili ya mchanga wa madini kuwasilishwa
Comments
Post a Comment