Posts

Man United watambulisha uzi mpya kwaajili ya msimu ujao

Image
 Manchester United mapemaa imeamua kuuweka hadharani uzi wake mpya wa msimu wa 2017/18. Uzi huo unaonekana kurudisha kumbukumbu ya Man United kuhusiana na jezi za enzo hizoo wakati wa kipindi cha Alex Ferguson na wachezaji kama Ryan Giggs walikuwa wakichipukia.

SABABU ZA SHILOLE KUKACHA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI KWA DENTI WA CHUO

Image
Msanii wa muziki wa kizazi wa Bongo Fleva na filamu, nchini Zuwena Mohamed maarufu kama  Shilole ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya matumizi mabaya ya mtandao kwa kuwa anaumwa. Leo (Jumatano) Shilole alipaswa kutoa ushahidi katika kesi hiyo inayomkabili mwanafunzi wa Chuo cha Bandari, Thomas Lucas (20) inayosikilizwa mbele ya Hakimu Boniface Lyamwike. Katika kesi hiyo, Lucas anakabiliwa na shtaka la mtandao kwa kumkashfu Shilole kupitia kwenye mtandao wa Instagram. Inadaiwa  kuwa mshtakiwa huyo alifanya hivyo wakati akijiua ni kosa na kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2016.  Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,2017 ambapo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Nandy: Wanaume wananisumbua sana

Image
MWANADADA anayefanya poa na ngoma yake ya One Day, Faustina Charles ‘Nandy’ amekiri kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware ambao wanahitaji penzi lake, lakini bila mafanikio. Akipiga stori na Za Motomoto News, Nandy alifunguka kuwa amekuwa akikumbana na vishawishi mbalimbali kwa ahadi kedekede ili tu waweze kutimiza azma yao lakini anajitahidi kupambana na hali hiyo sababu ameshajifunza kupitia kwa wenzake. “Usumbufu ni mkubwa mno kwa kweli, lakini siwezi kuwataja majina hata hao vigogo wanaonisumbua, mimi ni msichana ninayejielewa na wanaume wengi wamekuwa wakihaha kutaka kuonja penzi langu, wanagonga mwamba,” alisema.

Maalim Seif Aibukia Kanisani Kwa Askofu Gwajima

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad (kushoto) akiwa na  Mchungaji wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, Askofu Josephat Gwajima. LEO Mei 10, 2017, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad amekwenda kumtembelea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, kanisani kwake Ubungo, Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo ya faragha na Maalim Seif, Askofu Gwajima amesema ujio wa kiongozi huyo kanisani hapo ulikuwa ni kwa ajili ya kubadilishana mambo mbalimbali kuhusu nchi na mahusiano yao. “Maalim Seif ni rafiki yangu, ni siku nyingi tulikuwa hatujaonana, tumezungumzia mambo ya nchi mbalimbali na mahusiano yangu mimi na yeye. “Unaweza kuwa na rafiki ambaye anafanya kazi tofauti na yako, anaweza kuwa daktari na wewe ukawa siyo daktari, hata serikali haikatazi urafiki. “Nimemuuliza ni kipi kimempata Profesa (Lipumba) mpaka anavuruga chama chake, amenielezea ili na mim

APATA BWANA BOKO HARAM, AGOMA KURUDI NYUMBANI

Image
Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameshangaza wengi baada ya kuamua kubaki na mwanaume wa kundi hilo anayedai ni mumewe baada ya yeye na wenzake kuachiwa huru Jumamosi iliyopita. Msemaji wa Ikulu, Nigeria, Garba Shehu amenukuliwa akisema kuwa wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao amesema; “Hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.” Kutokana na uamuzi wa binti huyo, kundi la Boko Haram liliwaachia huru wasichana 82 baada ya mazungumzo kati yao na shirika la ICRC. Wapiganaji hao wanadaiwa kuwazuia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.

Waziri wa Katiba na Sheria atajwa sakata la watumishi wenye matatizo ya vyeti

Image
Sakata la watumishi wa umma waliofanyiwa uhakiki wa vyeti limezidi kuchukua sura mpya kila iitwapo leo ambapo awamu hii, Waziri wa serikali ya awamu ya tano amebainika kuwa miongoni mwa watumishi ambao vyeti vyao vina utata. Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ametajwa katika orodha ya watumishi ambao vyeti vyao vina matatizo ambapo uhakiki wake ulifanyika wakati akiwa mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na kisha waziri. Waziri Prof. Kabuni ambaye amebobea katika sheria, pamoja na waafanyakazi wengine wa UDSM wametajwa katika orodha ya watumishi wa umma ambao vyeti vyao havijakamilika. Katika orodha aliokabidhiwa Rais Dkt Magufuli na Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, jumla ya watumishi 9,932 walikutwa na vyeti vya kughushi, huku wengine zaidi ya 1,500 wakiwa na vyeti vyenye utata na wengine walikuwa wamepelek

HIZI NDIZO SABABU ZA TRUMP KUMFUTA KAZI MKURUGENZI WA F.B.I

Image
Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema. Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey ameondolewa katika nfasi yake. Hatahivyo wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi. Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita. Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo. Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika. Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza m

LEMA Ahoji Kushikiliwa kwa Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent Ambayo Wanafunzi Wake 35 Wamefariki na Ajali ya Basi.

Image
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Omog afunguka mambo mawili yatakayo ikwamisha Simba kuwa bingwa

Image
Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, ametamka kuwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara bado mgumu huku akitaja sababu mbili zitakazokwamisha taji hilo kutua Msimbazi. Kauli hiyo, aliitoa mara baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon, mchezo uliopigwa wikiendi hi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba yenye pointi 62, inachuana vikali na mabingwa watetezi Yanga wenye 59 wakiwa wamebakisha michezo minne kabla ya mchezo wao wa jana, tofauti na wapinzani wao ambao wamebakiza miwili. Omog alisema changamoto ya kwanza wanayokabiliana nayo ni kutoka kwa timu pinzani zilizopo kwenye hatari ya kushuka daraja ambazo zinapambana kubaki katika ligi kuu. Omog alisema, timu hizo zinaonyesha upinzani mkubwa katika mechi ambazo wanaendelea kukutana nazo, hali inayompa hofu ya kutwaa taji hilo. Aliongeza kuwa, kingine kinachompa hofu ya ubingwa ni presha ya wachezaji na viongozi kwenye timu ya kuwa na kiu ya ubingwa hali inayosababisha wawe wa

MENEJA BABU TALE AFUATA NYAYO ZA DOGO JANJA

Image
Baada ya hitmaker wa ngoma ya Kidebe,  Dogo Janja  kutamba katika mitandao ya kijamii siku chache zilizopita huku akijitapa kuwa yeye ndio msanii ambaye anapendeza kuliko wote hapa Tanzania, round hii ni zamu ya meneja wa Tiptop Connection na WCB Hamisi Tale a.k.a  Babu Tale . Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram  Babu Tale  alipost picha iliyomuonyesha akiwa na  Dogo Janja  na kuandika caption ambayo iliwaacha wengi midomo wazi. Caption ya  Babu Tale  ilisomeka kama  “Mpuuzi atabisha mimi ndio Manager wa kwanza Tanzania nzima kwa kupendeza na niko na msanii kwa kupendeza  @dogojanjatz”

Lundenga kuzuiwa kuandaa Miss TZ

Image
SERIKALI imetishia kuifuta Kampuni ya Lino Agency katika uandaaji wa shindano la Miss Tanzania ikiwa itashindwa kutoa zawadi kwa mshindi wa mwaka 2016/17, Diana Edward. Akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake bungeni mjini hapa juzi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, aliitaka kampuni hiyo iliyo chini ya Mkurugenzi Hashim Lundenga kumkabidhi zawadi ya gari Diana mara moja kabla serikali haijachukua hatua zaidi. Diana alitwaa taji hilo Oktoba 26, mwaka jana katika fainali ya shindano hilo lililofanyika jijini Mwanza. Wambura alisema kampuni hiyo inapaswa kutoa zawadi kwa mrembo huyo kufikia Juni mwaka huu. Naibu Waziri huyo alisema iwapo kampuni hiyo itashindwa kutii agizo hilo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuiondoa katika uandaaji wa shindano hilo. Mbali na zawadi ya Diana, Naibu Waziri huyo alisema kampuni hiyo pia inapaswa kuwapa zawadi warembo wengine waliofanya vizuri katika shindan

WAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI ZINGATIENI MIPAKA YA MADARAKA YENU-MAJALIWAWAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI ZINGATIENI MIPAKA YA MADARAKA YENU-MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa baada ya kufungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Selemani Jafo na kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja. Aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme baada ya kufungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Seriklali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, O

Mbunge Australia aweka historia, anyonyesha mtoto bungeni

Image
Senator kutoka jimbo la Queensland nchini Australia, Larissa Waters, ameweka historia bungeni hapo alipomleta kazini na kumnyonyesha mwanaye wa miezi miwili ikiwa ni mara ya kwanza na hivyo kutengeneza historia hiyo nchini humo. Larissa Waters amerejea kazini baada ya likizo ya uzazi na mwanaye huyo, huku akiwa tayari kutumia uhuru wake wa sheria mpya inayowaruhusu wazazi ambao ni senator,nchini Australia kuja na vichanga vyao na vilevile kuwanyonyesha punde wanapopatwa na njaa.

Msukuma awaumbua wabunge, adai walienda kwa waganga wakati wa uchaguzi

Image
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (ambaye ni mwakilishi wa waganga wa kienyeji Bungeni amesema karibia wabunge wote waliopo bungeni isipokuwa wabunge wawili tu ndiyo hawakupita kwa waganga wa kienyeji kipindi cha uchaguzi Mkuu 2015. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma akihotubia katika moja ya mkutano wake kipindi cha kampeni za Uchaguzi 2015. Msukuma amedai kuwa wabunge hao baada ya kupita katika chaguzi zao wamekuwa wakiwasahau waganga hao wa kienyeji na kufikia hatua ya kuwatumia polisi ili wawakamate badala ya kuwasaidia, hivyo Mbunge huyo ameiomba serikali japo kuwajengea hata chuo tu waganga hao wa kienyeji kwa kuwa wamekuwa wakifanya mambo mengi yanayosaidia katika jamii. "Nimekuwa nikisikia wabunge wakiwatetea sana wasanii humu ndani wanawasahau waganga wa kienyeji. Kwa karama niliyonayo nikiwaangalia Wabunge humu ndani wakati wa uchaguzi wote hakuna ambaye hakupita kwa waganga wa kienyeji, labda wawili ambao hawakupita kwa waganga a

Vilio vya Mastaa kwa Wanafunzi Waliokufa Arusha

Image
M AJONZI yamegubika nchi nzima kufuatia tukio la kihistoria la ajali ya basi lililosababisha vifo vya wanafunzi 33, walimu wawili na dereva iliyotokea Karatu mkoani Arusha. Taarifa zinasema kuwa basi hilo aina Toyota Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi, walimu na dereva ambalo ni mali ya Shule ya Lucky Vincent liliacha njia na kutumbukia katika Mto Marera uliyopo kilometa 25 kutoka kwenye geti la Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Mbali na ajali hiyo kuwagusa wengi ndani na nje ya nchi, mastaa kutoka kwenye tasnia mbalimbali nchini wameibuka na kuzungumza na Wikenda, wakiweka wazi hisia zao za namna walivyoguswa na ajali hiyo. Wasikie; PROFESA JAY: Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi. Kiukweli hili ni pigo kubwa sana kwa taifa letu, natoa pole sana kwa ndugu, jamaa wa marehemu na viongozi wote wa Mkoa wa Arusha kwa msiba huu mkubwa. Kwa mara nyingine tena kama taifa tunapoteza watoto wetu kwa idadi kubwa sana ambao wangeweza kuja kuwa hazina kubwa kwa

LIVE: Yanayojiri Arusha Kuaga Miili ya Wanafunzi Waliofariki kwa Ajali

Image
Makamu wa Rais wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan (kushoto) ,  akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (kulia), Mrisho Gambo,   baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  atakapoongoza  wananchi wa Mkoa wa Arusha na Watanzania  kuaga miili ya wanafunzi, na waalimu waliofariki kwenye ajali ya gari juzi Karatu.  Tukio  hilo linafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Jeshi la Wananchi na polisi wakiwa uwanjani katika taratibu za  kupokea miili ya wanafunzi waliofariki. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi kwa wafiwa na Watanzania wote. Viongozi wa dini,  watakaoendesha ibada  wamewasili mahali pa tukio ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali mkoani, akiwemo Waziri wa Fedha na Mipano Philip Mpango. Pia kuna walimu 30 kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Vikosi vya usalama vikiwa eneo litakalofanyika hafla ya kuwaaga marehemu. Uwanja wa Sheikh Amri Abaid umejaa watu  ambapo viko

Picha za wanafunzi 32 waliofafiki katikia ajali Arusha

Image
Juzi wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha walifariki dunia majira ya saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Gwajima ataka Bunge lisimame kuombeleza vifo vya wanafunzi 32

Image
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephath Gwajima amemtaka Spika wa Bunge kuahirisha kikao cha Bunge siku ya kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya jana. Amesema kama Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliamuru viongozi kusimama kwa kuwakumbuka watoto hao itakuwa ajabu kwa bunge kuendelea na vikao vya Bunge Amesema Spika akiahirisha Bunge kwa siku moja itatoa nafasi kwa wabunge hao kwenda Arusha ili kuomboleza pamoja.

NJAA YAMNYIMA SUBIRA MBUNGE WA CCM AFUNGUKA MBELE YA POLEPOLE

Image
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Mh. Flatei G. Massay  Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay amemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa. Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama,  kusikiliza kero na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Mbulu. Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei kubwa ya vyakula wanavyonunua kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivyo Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu. Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula. “Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula cha bei nafuu na siyo kile chakula cha bure,”

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Kuongoza Kuaga Wanafunzi Waliofariki Arusha Kesho

Image
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu kesho saa mbili asubuhi ataongoza wakazi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Abeid Karume kuaga miili ya wanafunzi waliofariki katika ajali ya gari Arusha ambapo serikali imegharamia sanda  na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vincent waliopoteza maisha jana kwenye ajali. Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro,  amesema taarifa za awali zinaonyesha tayari serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda za kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa heikh Amri Abeid. Mazingira ya shule hiyo. Aidha Lazaro amesema viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vincent  kwa ajili ya kikao.