WAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI ZINGATIENI MIPAKA YA MADARAKA YENU-MAJALIWAWAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI ZINGATIENI MIPAKA YA MADARAKA YENU-MAJALIWA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina
mjini Dodoma Mei 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za
Mitaa baada ya kufungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Hazina mjini
Dodoma Mei 9, 2017. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais,
Selemani Jafo na kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,
Profesa Joseph Semboja. Aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Mjini, Christina Mndeme.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,
Christina Mndeme baada ya kufungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri za Seriklali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina
mjini Dodoma Mei 9, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi
ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,
Profesa Joseph Semboja baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina
mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Selemani Jafo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………….
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Halmashauri nchini kuzingatia mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha
hatua wanazochukua katika utendaji wao zinafuata Sheria ,Kanuni na
Taratibu katika Utumishi wa Umma.
Ametoa
kauli hiyo leo (Jumanne, Mei 9, 2017) wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya katika ukumbi wa
Hazina mjini Dodoma.
Amesema
viongozi hao wanatakiwa kusimamia kikamilifu nidhamu katika Utumishi wa
Umma kwa sababu wenyewe ni kioo katika kuishi kwa kuzingatia miiko ya
Utumishi wa Umma.
Aidha,Mh.
Waziri Mkuu amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na
kuendelea kuwaimarisha zaidi katika kusimamia shughuli za Serikali na
maendeleo kwenye maeneo yao.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kutoa kipaumbelea
katika kufuatilia na kusimamia kwa makini sekta za afya, kilimo, elimu
na maji kwa kuwa ndizo zinazogusa zaidi maisha ya wananchi .
Pia
amewaelekeza wasimamie na kuziba mianya yote ya upotevu wa dawa katika
vituo vya kutolea huduma za afya na kudhibiti migogoro ya wakulima na
wafugaji pamoja na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira katika
maeneo yao.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa-TAMISEMI, Mheshimiwa Suleiman Jafo amesema lengo la mafunzo
hayo ni kuhakikisha viongozi hao wanapata mafanikio makubwa katika
utendaji wao wa kazi ili Serikali iweze kupata tija.
Awali
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja
alisema wametoa mafunzo kwa viongozi hao ili kuwajengea uwezo wa
kuongoza kwa kuwa mazingira ya kufanyia kazi na mbinu za kungoza
zinabadilika.
Alisema
mafunzo hayo yatatolewa kwa awamu nne kupitia kanda nne tofauti ambapo
awamu ya kwanza imeanza na kanda ya kati na imehusisha mikoa sita ya
Dodoma, Kigoma, Katavi, Tabora, Morogoro na Singida na awamu nyingine
zitakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Comments
Post a Comment