Nandy: Wanaume wananisumbua sana

MWANADADA anayefanya poa na ngoma yake ya One Day, Faustina Charles ‘Nandy’ amekiri kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware ambao wanahitaji penzi lake, lakini bila mafanikio.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Nandy alifunguka kuwa amekuwa akikumbana na vishawishi mbalimbali kwa ahadi kedekede ili tu waweze kutimiza azma yao lakini anajitahidi kupambana na hali hiyo sababu ameshajifunza kupitia kwa wenzake.

“Usumbufu ni mkubwa mno kwa kweli, lakini siwezi kuwataja majina hata hao vigogo wanaonisumbua, mimi ni msichana ninayejielewa na wanaume wengi wamekuwa wakihaha kutaka kuonja penzi langu, wanagonga mwamba,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog