Waziri wa Katiba na Sheria atajwa sakata la watumishi wenye matatizo ya vyeti

Sakata la watumishi wa umma waliofanyiwa uhakiki wa vyeti limezidi kuchukua sura mpya kila iitwapo leo ambapo awamu hii, Waziri wa serikali ya awamu ya tano amebainika kuwa miongoni mwa watumishi ambao vyeti vyao vina utata.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ametajwa katika orodha ya watumishi ambao vyeti vyao vina matatizo ambapo uhakiki wake ulifanyika wakati akiwa mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na kisha waziri.

Waziri Prof. Kabuni ambaye amebobea katika sheria, pamoja na waafanyakazi wengine wa UDSM wametajwa katika orodha ya watumishi wa umma ambao vyeti vyao havijakamilika.

Katika orodha aliokabidhiwa Rais Dkt Magufuli na Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, jumla ya watumishi 9,932 walikutwa na vyeti vya kughushi, huku wengine zaidi ya 1,500 wakiwa na vyeti vyenye utata na wengine walikuwa wamepeleka vyeti pungufu kwenye uhakiki.

Akizungumza suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Mukandala alisema kwa Prof. Kabudi ametajwa katika orodha hiyo kwa sababu cheti chake cja kidato cha nne hakikuonekana wakati wa uhakiki. Aidha, Prof. Mukandala alisema kuwa tayari Prof. Kabudi ameshawasilisha cheti hicho na kwamba watakipeleka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa ajili ya uhakiki.

Wakati Rais Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uhakiki wa watumishi wenye vyeti feki alisema kuwa, kwa wale ambao wanavyeti pungufu, wanaendelee kubaki kazini lakini uhakiki ufanyike vizuri kwa sababu si kila mtu alipita kidato cha sita kiweza kufika chuo. Hivyo kama hakupita kidato cha sita alafu ukamwambia akuletee cheti, hatokuwa nacho.

Comments

Popular posts from this blog