HIZI NDIZO SABABU ZA TRUMP KUMFUTA KAZI MKURUGENZI WA F.B.I
Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi mkurugenzi wa
shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala
la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat
Hillary Clinton, mamlaka imesema.
Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey ameondolewa katika nfasi yake.
Hatahivyo wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa
kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump
na Urusi.
Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey
alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la
Congress wiki iliopita.
Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba
alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba
ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.
Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.
Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja.
Naye kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la
Seneti, Bwana Chuck Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua
kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na
Urusi.
Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa
Comments
Post a Comment