Zitto amsifu Peneza kubadili taswira ya bajeti
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amempongeza Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Kigoma Upendo Peneza (CHADEMA) kuwa amefanikiwa kuacha alama ndani ya bunge la Tanzania akiwa na muda mfupi ndani ya bunge. Zitto ametoa pongezi hizo ambapo amesema Peneza anaingia katika rekodi za Wabunge waliotumia nafasi yao kushawishi jambo lenye faida kubwa kwa jamii na likafanikiwa ikiwa ni baada ya Serikali kutangaza kuondoa kodi ya VAT kwenye Taulo za Kike zinazotumika na Wanawake kipindi cha hedhi. “Kumekuwa na juhudi za kuleta mabadiliko haya miaka mingi kutokana na kazi za Mashirika kama TGNP Mtandao, SNV, Msichana Initiative nk. Upendo, licha ya kuwa na miaka 2 tu Bungeni aliweza kubeba hoja hii na kuiingiza Bungeni na kuunganisha Wabunge wote kutoka Vyama vyote.” ameandika Zitto Ameongeza “Licha ya kwamba kampeni yake ilikuwa ni Watoto wa shule wapewe Taulo hizi bure ( litafika tu hilo kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa ), amepata mafanikio