Ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh awamu ya pili waendelea kutekelezwa kwa zaidi ya aslimia 80- Mbulu
muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha Afya Dongobesh likiwa katika hatua ya ukamilishaji
Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu inategemea kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha
Afya Dongobesh ifikapo Juni 30 2018, hatua hii imefikiwa ikiwa ni utekelezaji
wa kiwango cha aslimia 80 kilichobainishwa
baada ya kufanyika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh,tathimini
hiyo ilitolewa na timu ya Wataalam toka
Tamisemi, wakilishirikiana na wataalam toka Mkoa wa Manyara.
Timu hizo
ziliweza kufanya ukuaguzi wa majengo hayo mapya yanayoendelea kukamilishwa kabla
ya Mwezi Juni kukamilika ili kubaini kama kiasi cha fedha Tsh. Milioni 400 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya
ujenzi wa majengo hayo unakamilika kwa wakati. Mgawao huo wa fedha uliotolewa
ikiwa na mgawao awamu ya pili baada ya maeneo mbalimbali nchini kupokea mgawo
wa awali.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akiteta jambo na wataalam waliofika kituoni hapo kwa ajili ya ukaguzi.
Sambamba na
ukaguzi huo timu hiyo haikusista kutoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya nchini ya Mkurugenzi wake ndugu Hudson
Kamoga kwa kusimamia ipasavyo fedha zinazotolewa na Serikali na kuwataka
kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati licha
ya kuchelewa kuanza ujenzi kutokana na kuchelewa kupata mgawao wa fedha.
Kazi ya ukaguzi jengo la mtumishi ikiwa imekamilika kwa wataalam mbalimbali toka Tamisemi, Mkoani, Wilayani na Wajumbe kushiriki kwa pamoja.
Kituo cha
Dongobesh kilipokea kiasi hicho cha fedha ili kujenga majengo matano ambayo ni Jengo la Upasuaji, Jengo la Maabara, Jengo
la Mama na Mtoto, Jengo la Kuhifadhi Maiti na Jengo la Mtumishi, Ujezi huo
unafanyika kwa kutumia nguvu ya wananchi
(force Account) ambayo hutoa fursa kwa jamii husika kufaidika na kazi kwa
malipo yaliyotolewa.
muonekano wa jengo la upasuaji kama jinsi linavyoonekana katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Aidha wajumbe
wa kamati inayosimamia ujenzi huo wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa
kutoa fedha hizo ambazo zimeweza kuleta mabadiliko makubwa katika kituo hicho kwani wananchi wa kata nzima wanategemea kituo
hicho kwa ajili ya kupata matibabu kituoni hapo na hivyo wameimbo Serikali kuendela kutoa
msaada mbalimbali ya fedha na Vifaa tiba ili kuboresha kituo na kutoa tiba
iliyo bora zaidi kuepusha vifo visivyo na lazima.
wajumbe wakiwa katika moja ya majengo yanayoendelea kujengwa ili kuona ujenzi umefikia kiwango gani.
Comments
Post a Comment