Mzee Ali Hassan Mwinyi akitoa nasaha zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu.
Mzee
Ali Hassan Mwinyi (kulia) akijumuika na waumini wengine wa Dini ya
Kiislam katika
swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum akitoa nasaha zake kwa waumini
wa dini ya Kiislamu.
Taswira ya baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ilivyoonekana.
Meneja wa
Kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiwa
ameungana na
waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika swala ya Eid El
Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam.
Meneja wa
Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati) akisalimiana na mmoja wa
waumini
baada ya kumalizika kwa swala ya Eid El Fitr.
Sehemu ya waumini akinamama waliojitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Waumini wakiomba dua.
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mapema leo Ijumaa
amewaongoza waumini wa Kiislamu katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El
Fitr, katika swala ya Eid El Fitr iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waumini mara baada ya swala hiyo, mzee Mwinyi
amewataka Waislamu kote nchini kusherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya
matendo mema ya kumpendeza Mwenyezi Mungu na kuliombea taifa ili amani
iliyopo iendelea kudumu milele.
“Waumini wa Dini ya Kiislam muendeleze ushirikiano,umoja na
mshikamano na madhehebu mengine ya dini nchini, pia mwendeleze kudumisha
matendo mema kama mlivyofanya kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani,”amesema.
source;GPL
Comments
Post a Comment