Breaking News: Moto Mkubwa Waibuka Kariakoo
Moto ukitekeleza ghorofa ya juu ya jengo hilo eneo la Kariakoo.
MOTO mkubwa umeibuka Kariakoo katika mitaa ya Livingstone na Aggrey
na unaendelea kuteketeza maduka. Tayari vikosi vya zimamoto vipo eneo la
tukio kupambana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo la ghorofa
ambalo lina maduka katika ghorofa ya chini.Moto huo ulianzia kwenye ghorofa ya kwanza katika jengo hilo lenye ghorofa mbili ambako kulikuwa na stoo ya vitu mbalimbali ambavyo vimeteketea kwa moto huo ambao moto huo ulielekea katika ghorofa ya juu.
Chanzo cha moto huo hadi tunakwenda mitamboni kilikuwa hakijajulikana.
Wakazi wa Dar es Salaam wakishuhudia moto huo.
Comments
Post a Comment