Nape Nnauye: Bora mnilaumu kwa 'Bao la mkono' sio kwa hili la Jamii Forums


Mbunge Mtama, Nape Nnauye amejikutaka akijibu hoja mbali mbali mtandaoni kufuatia mtandao wa Jamii Forums kusitisha kutoa huduma.

Utakumbuka Jamii Forums wamefikia hatua hiyo kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018.

Sasa Nape Nnaye alianza kueleza hisia zake kuhusu hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter; Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!.

Baada ya tweet hiyo idadi kubwa ya wachangia walionekana kuomnyooshea kutokana kipindi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016

Hata hivyo Nape aliwataka wachangia kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti.

“Nimeuliza hili swali toka mwanzo kina uhusiano gani wa hizi sheria mbili? Au tunakaririshwa au hatujui tunachotaka kusema,” alijibu Nape na mjadala kuendelea.

Utakumbuka katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 2015 wakati Nape Nnaye akiwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndipo alipoeleza kuwa chama hicho kingeshinda uchaguzi huo hata kwa bao la mkono kauli ambayo iliiubua mjadala mpana.



Comments

Popular posts from this blog