UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI


TAARIFA zinazosambaa mitandaoni zikisema mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Maria Godian Soko amefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Ubungo Riverside, Dar es Salaam, akiwa anakimbizwa hospitali kwa matatizo ya ujauzito, zimekanushwa na Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika chuo hicho, Hussein Amri Aman, aliyesema kwamba kwamba marehemu hakuwa na tatizo hilo.

Amri amesema  marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu kwa muda mrefu,  hali iliyokuwa ikisababisha apoteze fahamu, na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa (ambulance).

Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia, majira ya saa mbili kasoro usiku tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa Mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi”

Ameongeza: “Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya chuo zinaendelea ndipo ajali mbaya ikatokea pale River Side, taarifa zinazoendelea kusambaa kwamba marehemu alikuwa mjamzito anaenda kujifungua sio za kweli”.

Katika ajali hiyo hadi sasa walioripotiwa kufariki ni wanafunzi wawili ambao ni Maria Godian Soko (mwaka wa kwanza COSS) na Steven E Sango  (CPE CoET mwaka wa pili)  na dereva James.

Mwanafunzi mwingine aliyekuwepo katika msafara huo ni Abishai Nkiko (Bsc Industrial Engineering mwaka wa 3 CoET) hali yake ni mbaya na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

Maria Godian Soko ( B.A in psychology mwaka wa kwanza) amefariki jana usiku baada ya ambulance ya chuo kugongana na lori majira ya saa mbili  maeneo ya riverside -Ubungo  wakati alipokuwa akikimbizwa hospitali  baada ya kubanwa na pumu hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

Comments

Popular posts from this blog