Posts

Ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh awamu ya pili waendelea kutekelezwa kwa zaidi ya aslimia 80- Mbulu

Image
muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha Afya Dongobesh likiwa katika hatua ya ukamilishaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inategemea kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha Afya Dongobesh ifikapo Juni 30 2018, hatua hii imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa   kiwango cha aslimia 80 kilichobainishwa baada ya kufanyika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Dongobesh,tathimini hiyo ilitolewa na   timu ya Wataalam toka Tamisemi, wakilishirikiana na wataalam toka   Mkoa wa Manyara .   Timu ya wataalam wakiwa katika moja ya majengo mapya ya kituo cha afya wakiendelea na ukaguzi. Timu hizo ziliweza kufanya ukuaguzi wa majengo hayo mapya yanayoendelea kukamilishwa kabla ya Mwezi Juni kukamilika ili kubaini kama   kiasi cha fedha Tsh.   Milioni 400   zilizotolewa   na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo unakamilika kwa wakati. Mgawao huo wa fedha uliotolewa ikiwa na mgawao awamu ya pili baada ya maeneo mbalimbali

Breaking News: Moto Mkubwa Waibuka Kariakoo

Image
Moto ukitekeleza ghorofa ya juu ya jengo hilo eneo la Kariakoo. MOTO mkubwa umeibuka Kariakoo katika mitaa ya Livingstone na Aggrey na unaendelea kuteketeza maduka. Tayari vikosi vya zimamoto vipo eneo la tukio kupambana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo la ghorofa ambalo lina maduka katika ghorofa ya chini. Moto huo ulianzia kwenye ghorofa ya kwanza katika jengo hilo lenye ghorofa mbili ambako kulikuwa na stoo ya vitu mbalimbali ambavyo vimeteketea kwa moto huo ambao moto huo ulielekea katika ghorofa ya juu. Chanzo cha moto huo hadi tunakwenda mitamboni kilikuwa hakijajulikana. Vikosi vya Zimamoto vikiendelea na kazi Wakazi wa Dar es Salaam wakishuhudia moto huo.

Je,wajua Rais Kim alisafiri na choo chake mpaka Singapore?

Image
Imebainika kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisafiri na choo chake maalumu wakati wa mkutano wake na Rais Trump nchini Singapore. Sababu ya Kiongozi huyo kusafiri na choo chake imetajwa kuwa ni kuzuia kinyesi cha Kiongozi huyo kufanyiwa upembuzi na watu wa usalama wa mataifa mengine. Aidha imeelezwa kuwa Kiongozi huyo amekuwa na tabia ya kutembea na choo chake kila mahala anapokwenda kwani huwa hapendi kutumia vyoo vya umma. Kwa upande mwingine Kiongozi huyo alibeba gari lake aina ya Limousine ambalo halipitishi risasi pamoja na chakula chake mpaka nchini Singapore.

Ukeketaji Manyara yaongoza

Image
Hali ya Ukeketaji mkoa wa Manyara imefikia asilimia 70.8 kutoka asilimia 58 mwaka jana,hali ambayo ni mbaya zaidi licha ya jitihada za serikali na Mashirika binafsi kutoa elimu juu ya madhara ya kufanya ukeketaji. Hali ya Ukeketaji katika mkoa wa Manyara bado ni tatizo kutokana na watoto wachanga pia kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa siri pale wanapozaliwa. Anna Emmanuel Fisoo afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Manyara anaeleza kuwa tatizo la ukeketaji kwa wanawake na watoto bado lipo katika maeneo mengi ya mkoa katika baadhi ya makabila ya wafugaji. Amesema ukatili mwingine wanaofanyiwa watoto ni ulawiti na kubakwa na kwamba kesi nyingi zipo Mahakamani. Amesema ili kutokomeza ukatili huo ni lazima jamii,taasisi za serikali na mashirika binafsi kila mmoja atimize wajibu wake kwa wakati na kwa kufanya hivyo hali hiyo itakuwa imepungua kwa asiliamia 50 ifikapo mwaka 2022. Paskalia Changala Mratibu wa shirika linalojishughulisha na masuala ya kutokomeza ukeke

Lynn: Kuolewa na Diamond Wala Sina Papara

Image
Irene Charles ‘Lynn’ VIDEO Queen Irene Charles ‘Lynn’ ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema ametulia na hana papara kwani kama Mungu amepanga aolewe na msanii huyo, lazima itokee! Akizungumza na Risasi Jumatano, Lynn alisema, hawezi kuleta drama kwenye mitandao kuhusiana na suala lake na Diamond ila anachojua yeye kama Mungu amepanga aolewe naye, itakuwa hivyo na kama siyo basi ataolewa na mwingine aliyepangiwa. “Unajua siku zote ndoa hupangwa na Mungu hivyo kama Dai (Diamond) alipangwa kuwa wangu basi atakuwa wala sina papara, kama hajapangwa kuwa wangu atakuja mwingine,” alisema Lynn.

Tabia Ya Kuzoeana inavyoweza kuathiri Maisha yako ya kimahusiano

Image
Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla. Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini. Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinn

Breaking News: Madrid Wamtangaza Lopetegui Kuwa Kocha Mpya

Image
Julen Lopetegui Klabu ya Real Madrid imemtangaza Kocha wa sasa wa Hispania, Julen Lopetegui kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo na atajiunga nayo baada ya mashindano ya Kombe la Dunia

Nape Nnauye: Bora mnilaumu kwa 'Bao la mkono' sio kwa hili la Jamii Forums

Image
Mbunge Mtama, Nape Nnauye amejikutaka akijibu hoja mbali mbali mtandaoni kufuatia mtandao wa Jamii Forums kusitisha kutoa huduma. Utakumbuka Jamii Forums wamefikia hatua hiyo kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018. Sasa Nape Nnaye alianza kueleza hisia zake kuhusu hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter; Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!. Baada ya tweet hiyo idadi kubwa ya wachangia walionekana kuomnyooshea kutokana kipindi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016 Hata hivyo Nape aliwataka wachangia kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti. “Nimeuliza hili swali toka mwanzo kina uhusiano gani wa hizi sheria mbili? Au tunakaririshwa au hatujui tunachotaka kusema,” alijibu Nape na mjadala kuendelea. Utakumbuka katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 2015 wakati Nape Nnaye akiwa Katibu Mwenezi

JPM Amwaga Tsh. Milioni 10 Cash Ujenzi wa Msikiti Dar

Image
RAIS John Magufuli ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 625 ya sementi itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco. Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au mei mwakani. “Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote,” amesema Rais Magufuli

UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI

Image
TAARIFA zinazosambaa mitandaoni zikisema mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Maria Godian Soko amefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Ubungo Riverside, Dar es Salaam, akiwa anakimbizwa hospitali kwa matatizo ya ujauzito, zimekanushwa na Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika chuo hicho, Hussein Amri Aman, aliyesema kwamba kwamba marehemu hakuwa na tatizo hilo. Amri amesema  marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu kwa muda mrefu,  hali iliyokuwa ikisababisha apoteze fahamu, na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa (ambulance). “ Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia, majira ya saa mbili kasoro usiku tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa Mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi” Ameongeza: “ Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya c

Historia Imeandikwa: Trump, Kim Jong Un Wakutana Live Singapore

Image
MKUTANO  wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani,  Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un,  umefanyika nchini Singapore. Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili  pekee yao na wakalimani wao. Mkutano huo ulianza kwa viongozi  hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao. Rais Trump amesema wawili hao wamepiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka za makubaliano. Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia. Hata hivyo, haijabainika ni nini kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini. Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo. Mkutano uliokuw

Kafulila kuelezea sakata la Tegeta Escrow

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema ataanza kuelezea kwa kina sakata lililotikisa nchi la kashfa ya Tegeta Escrow wiki ijayo kupitia gazeti la Uwazi. Akizungmza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Kafulila alisema amegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo wananchi wanataka kuyajua kuhusu sakata hilo, hivyo ameamua kuyaandika yote ili kiu ya Watanzania kujua kuhusu sakata hilo iishe. “Najua kwamba mimi ndiye niliyelibebea bango bungeni sakata lile na kwa kuwa Gazeti la Uwazi linasomwa na watu wengi, nimeamua kuyaeleza yote kupitia gazeti hili kuanzia toleo lijalo,” alisema Kafulila. Alifafanua kuwa wazo la kuandika sakata hilo amelipata baada ya kuulizwa sana na baadhi ya wananchi kwamba liliishaje na jinsi lilivyomfanya akorofishane na vigogo wengi na hata kujihatarishia maisha. “Kwa kuwa hilo ni jambo zito, ni vema wananchi wajiandae kusoma kwa urefu juu ya sakata hilo kwenye gazeti hili. Nadhani nimefanya uamuzi sahihi,” alisema Kafulila.

Ulinzi wa Rais wa Korea Kaskazini usipime

Image
Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore. Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote . Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka. Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji. Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri. Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi. Mwisho

Jafo amjia juu mkandarasi stendi ya mabasi Njombe

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameonyesha kukerwa kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha mji wa Njombe licha ya serikali fedha zote za gharama ya ujenzi huo zaidi ya Sh. bilioni 10. Ujenzi wa kituo hicho ulianza tangu Desemba 2013 lakini hadi sasa haijakamilika. Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemjia juu mkandarasi aliyepewa kazi hiyo pamoja na upande wa usimamizi wa ujenzi huo na kudai kuwa umechelewa kukamilika kutokana na uzembe wao. “Hapo awali kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na MASASI CONSTRUCTION kwa kujenga awamu ya kwanza na ya pili ambapo katika awamu hizo zimekamilika lakini kwa kuchelewa sana na kulazimika kutafutwa mkandarasi mwingine ili akamilishe awamu ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa mradi huo,”amesema. Amebainisha kuwa awamu ya tatu Halmashauri ya mji wa Njombe wamempata mkandarasi mpya ambaye ni kampuni ya HAINAN INTERNATIONAL na amesaini mkataba mwezi Mei 2018 na anatarajiwa ku

Breaking News: Waziri Mwigulu Amsimamisha Kazi Merlin Komba

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Waraka wa barua unaodaiwa kuandikwa na Serikali dhidi ya Makanisa unaosambaa mitandaoni si wa kweli na kwamba ni uhalifu umefanywa na watu wasioitakia nchi mema. Waziri Nchemba amesema Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa. Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo taarifa hiyo inayosambaa ni batili na tayari uchunguzi umeanza kufanyika. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jam

Kutembea haraka kunarefusha Maisha

Image
Leo June 8, 2018 nakusogezea Utafiti uliochapishwa katika jarida la “Mazoezi ya matibabu” huko Uingereza limefafanua uhusiano kati ya maisha marefu na kasi ya kutembea. Wanasayansi wa Uingereza na Australia wameelezea kwamba watu wanaotembea haraka si rahisi kupatwa na ugonjwa wa moyo. Imeonekana kwamba wale walio na umri wa miaka 60 au chini ya hapo ambao wanatembea haraka wamepunguza hatari ya kufariki kutokana na magonjwa ya moyo kwa asilimia 53. Watafiti wanasema kwamba kasi ya Kilomita 5 hadi 7 kwa saa ni ya kutosha. Madaktari wanaamini lengo kamili ni kuharakisha mapigo ya moyo na kutokwa na jasho wakati wa kutembea. Waendesha magari nchini Uingereza ambao hutumia angalau nusu saa kufanya mazoezi na kula vyakula vya afya basi hurefusha maisha kwa miaka kumi.

Mfumo Mpya wa Malipo Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuboresha Huduma kwa Wananchi

Image
Mfumo mpya wa malipo epicor toleo Na. 10.2 unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini umeelezwa kuboresha huduma kwa wananchi kutokana na kuwa wa uwazi na kurahisisha kazi kwa watumiaji wa mfumo huo. Akieleza lengo la uboreshaji wa mfumo huo leo, Jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Manunuzi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Dodoma, Arusha, Manyara na Singida, mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Agustino Manda amesema mfumo huo utapunguza kazi na kuongeza ufanisi wa kazi kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini. “Mfumo huu utaweka mambo wazi, watu watawajibika na mtumiaji wa mwisho ambaye ni mteja atapata huduma nzuri na kuridhika na huduma atakayopewa,” amesema Manda. Ameendelea kusema, lengo la kuboresha mfumo huo ni kutoa huduma nzuri kwa Wananchi, Wananchi kutochele

Maafisa Ugavi Waaswa Kuzingatia Sheria na Kanuni Katika Manunuzi

Image
Maafisa Ugavi Wametakiwa Kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu za Manunuzi ili kuleta thamani halisi ya fedha zinazotumika katika sekta hiyo ili halmashauri zote zitekeleze dhana ya kutoa huduma bora kwa wananchi. Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa maafisa hao leo Jijini Mbeya, Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw. Johnson Nyingi amewata  kuzingatia weledi na taratibu zote zinazosimamia sekta ya manunuzi kwa kuzingatia mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanayoendelea kwa mikoa ya Mbeya, Rukwa, Njombe na Songwe. Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia shughuli za Serikali, Idara ya Tawala za Mikoa Bw. Johnson Nyingi akifungua mafunzo kwa maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe leo Jijini Mbeya. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID