Breaking News: Waziri Mwigulu Amsimamisha Kazi Merlin Komba

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Waraka wa barua unaodaiwa kuandikwa na Serikali dhidi ya Makanisa unaosambaa mitandaoni si wa kweli na kwamba ni uhalifu umefanywa na watu wasioitakia nchi mema.

Waziri Nchemba amesema Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa.

Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo taarifa hiyo inayosambaa ni batili na tayari uchunguzi umeanza kufanyika.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo
Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

Comments

Popular posts from this blog