Posts

Saba Wafariki Ajalini Mkoani Kigoma

Image
Lori likiwa limepinduka. Hali ilivyokuwa mahali ilipotokea ajali. Mashuhuda wakitazama mabaki ya lori hilo. Watu saba wamefariki katika ajali iliyohusisha lori aina ya Scania lililokuwa likitokea kijiji cha Mkongoro mkoani Kigoma ambapo dereva wake alishindwa kulimudu wakati akishuka kwenye mteremko uliokuwa na kona kali na kumgonga mtembea kwa miguu na kisha likapinduka. Mkuu wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

ALIYETEKA NDEGE YA TANZANIA MWAKA 1982 KUMTAKA NYERERE AJIUZULU AFARIKI

Image
  Wakili nguli Yasin Memba anayedaiwa kuteka ndege ya Tanzania mwaka 1982 amefariki dunia jana Jumanne Machi 20, 2018 jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa wakili wa kujitegemea na mwanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) Mathew Kakamba, amesema Memba amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini humo. Memba ni miongoni mwa watanzania wawili wanaodaiwa kuteka ndege ya Tanzania iliyokuwa na abiria 90, Februari 1982 wakishinikiza Rais wa wakati huo, Julius Nyerere kujiuzulu. Chanzo - Mwananchi

BARAZA LA MITIHANI -NECTA LAFANYA MABADILIKO MTIHANI DARASA LA SABA

Image
Wanafunzi wa darasa la saba ambao watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa utungaji wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi . Mabadiliko hayo yamefanywa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) jana na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde. Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma. Nchimbi amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk). Amesema maswali 40 kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa. Kutokana na muundo huo mpya, Necta imetoa wito kwa walimu...

Faida 10 za kutumia Mafuta ya Nazi

Image
1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo: Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum. 2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula: Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa ...

Breaking News: Abdul Nondo Arudishwa Iringa, Apandishwa Kizimbani

Image
Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi, Abdul Nondo amerudishwa mkoani Iringa na kufikishwa Mahakama ya Wilaya. Awali Nondo alitolewa Iringa baada ya mahojihano na Polisi na kupelekwa Dar kwa Mkurugenzi wa Upelelezi makosa ya Jinai kwa mahojiano. Kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, amesema dhamana ya Nondo itatazamwa Jumatatu ijayo Machi 26, baada ya hakimu kuomba kusoma sheria inasemaje juu ya kuzuiwa dhamana kwake. Imeelezwa kuwa, Nondo amesomewa mashtaka kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo Mitandaoni na kosa la pili ni kudanganya kuwa alitekwa. Shauri limeahirishwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande.

Waziri Mwakyembe: Nimesikitishwa na matamshi ya Diamond

Image
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amesikitishwa na matamshi ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakati akihojiwa na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy, kwa hatua ambazo Wizara inachukua kulinda maadili ya Kitanzania katika tasnia ya sanaa. Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili, yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza anayemlaumu. Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake. Maamuzi ya Naibu Waziri ni maamuzi ya Wizara. Kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular he is. Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji w...

Wawili Mbaroni kwa Kuhamasisha Maandamano

Image
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia kwenye mitandao ya kijamii wakitumia simu zao za mikononi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Machi 21, 2018 na kuongeza kuwa watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana Aprili 26 mwaka huu

RC Makonda atoa ufafanuzi kuhusu tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ameshtusha na taarifa zilizosambaa mitanaoni kuhusu tukio la Afisa mmoja wa Ubalozi wa Syria ambaye amedaiwa kushambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha. Afisa wa Ubalozi wa Syria anayetajwa kushambuliwa na kuporwa fedha Mhe. Makonda ametoa taarifa yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa ambapo amewataka wananchi kutulia na vyombo vya usalama wanafuatilia kwa umakini tukio hilo. Soma taarifa hiyo hapa chini: TAARIFA YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA. Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha leo mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi. Nawaomba sana wananchi wa Da...

Waziri Shonza Kina Pretty Wapo Wengi, Bado Wanatamba!

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza. . KWAKO mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza. Habari na pole na majukumu yako ya kila siku. Najua Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli ni ya kazi. Watendaji wake mpo bize naweza kusema kuliko awamu zote zilizotangulia. Ukitaka kunijulia hali yangu, mimi ni mzima wa afya. Naendelea kupambana katika taaluma yangu ya uandishi wa habari. Mungu anasaidia bado tunaendelea kupambana na changamoto ya kuusuka uchumi wa nchi yetu. Baada ya salamu hizo, moja kwa moja niende kwenye dhumuni la mimi kukuandikia barua hii leo. Mheshimiwa waziri, hivi karibuni niliona ulivyomchukulia hatua msanii Pretty Kind kutojishughulisha na shughuli za muziki katika kipindi cha miezi sita. Nilifurahi kusikia hivyo maana nilijua kweli serikali ila dhamira njema ya kulinda maadili ya Mtanzania. Kuvaa nusu utupu si jambo jema na hakuna muungwana yeyote anayeweza kufurahia...

BREAKING NEWS: Rais Magufuli atengua uteuzi wa mwenyekiti wa NHC

Image
Rais Dkt. John Magufuli RAIS Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi Blandina Nyoni kuanzia leo tarehe 21 Machi 2018.

Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Apata Ajali Kigoma

Image
Gari alilokuwa akilitumia Mkurugenzi wa TBC baada ya kupata ajali. Watu wawili wamefariki dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma mjini jana. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu. Mkurugenzi wa TBC, Ayoub Rioba (kushoto) akiwa katika eneo la ajali na watu wengine. Kamanda Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Teresia Mpoma (55) mkulima na mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na majeruhi mmoja, Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambaye hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu. Amesema gari hilo lenye namba za usajili S...

Naibu Waziri Mavunde Kalazwa Morogoro

Image
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavundeakiwa kalala kitandani Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro akisumbuliwa na homa kali. Mavunde amesema alipelekwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia Jumapili baada ya kujisikia vibaya na saivi anaendelea kupatiwa matibabu

MTOTO ALIYECHOMWA SINDANO KIMAKOSA NA MADAKTARI KICHWANI,CHAANZA KUOZA

Image
Leo stori ninayokusogezea ni kuhusu matukio ya kutokuwa makini katika idara ya afya hasa kwa madaktari yanazidi kuzua wasiwasi kwa wananchi nchini Kenya, tukio lililotokea siku za hivi karibuni ni la mtoto kuchomwa dawa isiyofaa na kumfanya aanze kuoza kichwa. Tukio hili limefanyika katika hospitali ya Malava General Hospital katika jimbo la Kakamega na linatokea huku kukiwa na kesi dhidi ya Madaktari wa hospital ya Kenyatta inaendelea baada ya Daktari kumfanyia upasuaji mgonjwa asiyestahili. Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Clinton Luchivya alikuwa amepelekwa katika hospitali hiyo baada ya kuwa mgonjwa na madaktari kumchoma kichwani baada ya kukosa mshipa wa kumwekea dawa. Kulingana na mama wa mtoto huyo, mwanae alikuwa na ugonjwa wa Malaria kabla ya kupokea matibabu katika hospitali hiyo. Alisema kuwa mwanae alikuwa ameanza kubadilika badilika kabla ya kufahamu kuwa kichwa chake kinaoza.
Image
Huku Drama za Diamond na Wema Zikinoga, Kule Zari Bata Batani – Picha 7 WAKATI Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz akiendeleza drama ya mapenzi na aliyekuwa girl friend wake, Wema Sepetu kupitia mitandao ya kijamii, mzazi mwenzake na mwanamuziki huyo, Zari The Bosy Lady ameendelea kura raha katika Hoteli ya Sun City nchini Afrika Kusini anakoishi. Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram ametupia picha saba akila bata katika hoteli hiyo kuonyesha kuwa haumizwi na kile anachokifanya x wake huyo mitandaoni kwa kujiweka karibu na Wema, kupost picha na maneno yanayoonyesha kuwa wamerudisha uhusiano wao. Zari baada ya kuweka picha hizo hakuandika maneno mengi bali ameweka caption hii;  Sun City typa weekend. Kuanzia jana Ijumaa kumekuwa na drama mitandaoni zikionyesha Wema na Diamond kama tayari wamesharudiana baada ya Wema kutupia picha na kipande cha video mpya ya Diamond, African Beauty na kumfagilia boy friend wake huyo wa kitambo. Wema aliandika...

Mzee Mkapa Ataka Mjadala wa Kitaifa

Image
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa amesema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa. Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu na kumuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula. Mzee Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi ama ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa kuondoa ada kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne pamoja kuongeza madawati, nyumba za walimu, madarasa, vitabu, kulipa stahiki za walimu ...

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali ...