Posts

Wivu wa Mapenzi Wasababisha Mauaji ya Kinyama ya Watu wawili

Image
Watu wawili wamefariki dunia na mwingine mmoja kujijeruhi baada ya kutokea ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi mjni Bunda. Tukio hilo lilitokea jana saa tano asubuhi katika Mtaa wa Bunda Stoo baada ya mtu mmoja kuwavamia watu wawili kisha kuwachoma visu kabla ya kujichoma mwenyewe. Akizungumza mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed alisema jana kuwa waliouawa ni Daudi Phares (29) mkazi wa Bunda na msichana aliyetambulika kwa jina moja la Monica (22) mkazi wa Magu mkoani Mwanza. Kamanda huyo alimtaja aliyejijeruhi baada ya kujichoma kisu maeneo mbalimbali mwilini mwake kuwa ni Selemani Jeremia (33) ambaye ni mkazi wa Magu. Alisema kuwa siku ya tukio Selemani alisafiri kutoka Magu mkoani Mwanza hadi Bunda ambapo alifika nyumbani kwa Daudi na kumkuta akiwa na Monica. Baada ya kufika nyumbani hapo Selemani alianza kumchoma visu Dauidi katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo kifuani upande wa kushoto na kusababisha ki

MKUU WA WILAYA YA MBULU AAGIZA KITUO CHA POLISI KUJENGWA HARAKA.

Image
Mkuu Wa wilaya ya mbulu  chelestino s mofuga leo 09/10/2017 amekutana na wajumbe wa WDC  wa kata ya Eshkesh , kujadili maendeleo ya kituo cha polisi cha yaeda chini ambacho kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba 2017.  Mkuu huyo amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi kuwachukua maelezo na  kuahidi kusimamia kikamilifu  michango ya wananchi ili kujenga kituo hicho.  Mkuu wa wilaya aliunda tume kuchunguza matukio ya ujangili wa nyara za serikali, wizi wa mifugo na mauaji ya binadamu mnamo mwezi wa nne 2017, na moja ya mapendekezo ya uthibiti wa matukio ya uhalifu ni kujenga kituo cha polisi. Wajumbe hao wamebainika kusuasua kusimamia michango licha ya wananchi kuunga mkono ujenzi huo. Mkuu wa wilaya ametoa siku 30 kukamilisha michango ya ujenI wa kituo cha polisi.

Waziri wa afya afariki baada ya kukimbia

Image
Slim Chaker aliteuliwa waziri wa afya mwezi uliopita Waziri wa afya nchini Tunisia amefariki kutokana na mshutuko wa moyo baada ya kushiriki katika mbio za kuchangisha fedha za kusaidia kupambana na ugonjwa wa saratani. Slim Chaker, 56, aliugua baada ya kukimbia mita 500, kufariki kwenye hospitali ya kijeshi, kwa mujibu wa wizara ya afya. Waziri mkuu Youssef Chahed alisema kuwa amempoteza ndugu ambaye alikuwa akitoa huduma ya kibinadamu. Wanawake waislamu nchini Tunisia waruhusiwa kuolewa na wanaume wasio waislamu Mbio hizo ziliandaliwa kwenye mji wa pwani wa Nabeul siku ya Jumapili kuchangisha fedha za kujenga zahanati ya watoto ya kutibu ugonjwa wa saratani. Bwana Chaker aliteuliwa kuwa waziri wa afya mwezi uliopita wakati wa mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri.

Hallelujah ya Diamond yaweka rekodi Kimataifa Yatikisa Uingereza

Image
                Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake kila kukicha. Baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha Morgan Heritage kuweka rekodi kubwa ya kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 15, wimbo huo umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra ya nchini Uingereza. Hallelujah’ umeshika namba moja katika Top 5 ya kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ . Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri nchini humo ikiwemo na kwenye kituo kingine cha Capital Xtra.

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA ,GARI YA ABIRIA AINA YA HIECE LATUMBUKIA ZIWANI

Image
              Gari ndogo la abiria (hiace) likiwa na abiria limetumbukia ziwani wakati likijaribu kuingia kwenye kivuko cha Kigongo Ferry jijini Mwanza, watu watatu tu mpaka sasa wameokolewa Chanzo: Radio Free Afrika

SHAMSA FORD AZIDI KUMSHUKIA ILALA MJINGA,AMPA MAKAVU LIVE

Image
          UKITAKA kujua kichaa cha ‘Queen’ wa Bongo Muvi, Shamsa Ford, basi jaribu kuichokonoa ndoa yake, na hicho ndicho anachokifanya mtu mmoja aliyemfahamu kwa jina la Ilala Mjinga, ambaye kazi yake ni moja tu, kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuhusiana na ndoa yake na mumewe, Chid Mapenzi. Kwa mujibu wa Shamsa ambaye siku chache nyuma alisema kuwa anamuona jini-mkatakamba anainyapianyapia ndoa yake, hatimaye mambo yakamfika shingoni na kuamua kushusha waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwataka wale wote ambao wanadhani atakuja kuachana na mumewe, basi wajue kwamba hiyo ni ndoto sawa na kusubiri embe dodo kwenye mti wa korosho! NA ISRI MOHAMED/GPL Post Views: 22

Waziri Mkuchika awachimba biti watumishi

Image
Waziri, George Mkuchika amefunguka na kuweka wazi mipango yake katika kutumikia nafasi yake na kusema yeye ataanza kuhakikisha watumishi wa Umma wanatumia muda wao kufanya kazi na hataki kusikia watumishi wameondoka makazini kwenda kunywa chai. Waziri Mkuchika ambaye leo Oktoba 10, 2017 ameapishwa na Rais Magufuli kuwa Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kuwa katika kipindi chake atahakikisha wafanyakazi wanalipwa mshahara kulingana na kazi zao kweli, na wanatumia muda wa kazi kufanya kazi za serikali. "Kwanza katika kipindi changu nikiwa Waziri kwa watumishi wa Umma, nataka wananchi wanapofika maofisini wawakute maofisini, mara nyingi wengi wanaripoto ofisini baada ya muda wanaondoka wanasema wanaenda kunywa chai, yaani wananchi wanatoka vijijini wanamsuburi mtumishi aje eti ameenda kunywa chai jambo hili kuanzia leo nitasimamia kuhakikisha watumishi wa umma wanashinda kazini kwao ili kila mtumishi wa Umma alipwe ms

Mawaziri Wapya wa JPM Waanika Mikakati Yao, Sasa ni Mchakamchaka

Image
Mawaziri na Manaibu Waziri wakiapa, Ikulu Dar. MAWAZIRI na manaibu walioapishwa na Rais John Magufuli, wametoa ahadi ya jinsi watakavyotekeleza majukumu yao. Mawaziri na manaibu walioapishwa leo Jumatatu wametoa ahadi muda mfupi baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Waziri Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema atahakikisha watumishi wanakuwepo ofisini kuwahudumia wananchi. Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenda kunywa chai, hivyo atahakikisha wanabaki ofisini kutoa huduma. Kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Mkuchika amesema, “Nitatoa elimu na nitatumia muda wangu mwingi na ndugu zangu wa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa). Nitaongea na Waziri wa Elimu somo la rushwa lifundishwe kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.” “Ni wizara yenye changamoto nyingi, ng’ombe wanapigwa mnada, hawana maeneo ya malisho, viwanda vya mifugo na mchango wa maziwa ni tatizo, niko katika tafakari, nin

Diamond Platinumz awagaragaza Davido na Wizkid Afrimma 2017

Image
                Msanii wa muziki Bongo, Diamond ameibuka mshindi baada ya kunyakuwa tuzo ya Afrimma katika kipengele cha Best Artist of The Year. Tuzo hizo ambazo zimetolewa usiku wa kuamkia leo Taxes nchini Marekani, Diamond amewashinda wasanii kadhaa wakubwa wa Afrika kama Davido na Wizkid ambao walikuwa wakiwania tuzo hiyo katika kipengele kimoja kama inayonekana hapa chini;  Artist of The Year Flavour (Nigeria) Diamond Platnumz ( Tanzania) Fally Ipupa- Congo Wizkid (Nigeria) Cassper Nyovest (South Africa) Davido – (Nigeria) Eddy Kenzo – Uganda Tekno – Nigeria Mr Eazi – Nigeria C4 Pedro – Angola

Kichwa cha mwandishi aliyetoweka chapatikana baharini Sweden

Image
                 Kichwa cha mwandishi wa Sweden Kim Wall kimepatikana , miezi miwili baada ya kupotea katika ziara na raia mmoja wa Denmark. Waogeleaji walipata mifuko iliokuwa na kichwa chake, miguu na nguo katika eneo la Koge Bay kusini mwa mji wa Copennhagen kulingana na inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo Jens Moller Jensen. Vilipatikana karibu na pale mwili wa Wall ulipokuwa siku chache tu baada ya kupanda katika manuwari tarehe 10 Agosti. Bwana Marsden mwenye umri wa miaka 46 amekana kumuua bi Moller Jensen akisema mabegi hayo yaliopatikana yalikuwa yamechanganywa na kupimwa uzani na vipande vya vyuma. ”Jana alfajiri tulipata begi ambalo lilikuwa na nguo za Kim, suruali ya ndani na viatu.katika begi hilo hilo kulikuwa na kisu na kulikuwa na mabomba ya magari” . Matokeo ya uchunguzi yamebaini kwamba kichwa hicho ni cha bi Wall na kwamba hakina ishara za kwamba fuvu lake la kichwa liliumizwa ama hata kupigwa.   Matokeo hayo yanaenda kinyume na taarifa za

Sirro Asema Hataki Malumbano Kuhusu Kushambuliwa Lissu

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema hataki malumbano na hana majibu kuhusu shinikizo linalotolewa na Chadema na familia ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuruhusu vyombo vya nje kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi kwa mbunge huyo. IGP Sirro amesema hayo leo Jumapili jijini hapa, akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alipojibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kauli yake baada ya familia ya Lissu na viongozi wa Chadema kutamka kuwa hawana imani na Jeshi la Polisi kuhusu uchunguzi huo. Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alijeruhiwa kwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya. IGP Sirro amesema yeye na jeshi lake wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria kwa kuwatumikia Watanzania wote kuhakikisha wanakuwa sala

ZARI THE BOSS LADY AKATA MZIZI WA FITNA,AIBUKA NA KUJIBU YOTE LIVE

Image
                 Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu kama Zari The Boss Lady amefunguka na kudai kuwa yeye na mpenzi wake huyo hawajaachana. Akiongea katika U-Heard ya Clouds FM, Zari amedai kuwa hawajaachana kama inavyodaiwa na watu hii ni kutokana na kuwa hakumu-wish happy birtday katika mitandao ya kijamii kama ilivyozoeleka. Hakuna lolote baya linaloendelea kati yake na Diamond, na wanaheshima mikataba aliyonayo na kampuni pia hakuna chochote kibaya kinachoendele,” ameema mrembo huyo. Pia akaongeza kuwa “Nilimu-wish siku yake ya kuzaliwa sema nilitumia njia ya kawaida,na tunajaribu kuhamisha maisha yetu katika mitandao kuwa ya kawaida. Vile vile mrembo huyo alisisitiza kuwa stori zinazoenezwa kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond sio za kweli na kuhusu DNA pia sio kweli.

BREAKING NEWS : AJALI MBAYA YA GARI NA TRENI TANGA LEO

Image
Gari iliyokuwa kuwa imepakiza watoto imezima kwenye kivuko cha Kwaminchi na kugongwa na treni. Watoto wawili waliokuwa wamekaa mbele walinusurika kifo baada ya dereva kuwaambia waruke, ila waliumia na kukimbizwa Hospitali.

IGP SIRRO AWAJENGEA UWEZO ASKARI WA MBEYA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya, aliokutananao Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na kamanda wa Polisi mkoani humo (DCP) Mohamed Mpinga, wakiwa katika picha na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa baada ya kikao kazi cha kubadilishana uzoefu katika kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu aliloandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wa kutumia silaha za moto cha mk

CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI GIZA NENE, MADIWANI WALIOJIUZULU WATIMKIA CCM.

Image
Na Fredy Mgunda,Iringa. Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimalisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA. Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli. “Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao nah ii ndio mikakati yetu”alisema Rubeya Rubeya  aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukije

Mbowe ampongeza Rais Magufuli

Image
Babati.  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amepongeza kitendo cha Rais John Magufuli kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa kwa zaidi ya miaka saba kambi hiyo ilikuwa inaishauri Serikali kufanya hivyo. Mbowe amesema hayo leo Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda. Amesema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi. "Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," amesema Mbowe. Amesema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano. er 07, 2017 No comments Babati.  Mwenyekiti wa Chadema,

FT: TANZANIA 1-1 MALAWI kKUTOKA UWANJA WA UHURU

Image
Kikosi cha timu ya Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Malawi leo Uwanja wa Uhuru Dar. Kikosi cha timu ya Malawi. MPIRA UMEKWISHA Dk 90+4 Samatta yuko chini anatibiwa baada ya kugongana na beki wa Malawi wakati akijaribu kufunga, wote wametolewa nje kutibiwa Dk 90+2 Muzamiru analambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu ya pili kwa Taifa Stars Dk 90 nafasi nyingine ya Taifa, lakini kipa wa Malawi anaokoa Dk 90 nafasi nyingine ya Taifa, lakini kipa wa Malawi anaokoa Dk 88 Mbaraka Yusuf anapoteza nafasi akiwa yeye na lango, kazi nzuri ya Samatta ameshindwa kuitumia Dk 85, Nyoni amepewa kadi nyekundu, mwamuzi anamtuhumu kumpiga mwenzake kiwiko lakini mchezaji huyo wa Malawi, hakuadhibiwa kwa kuwa alimvamia Nyoni Dk 83 Abdul Hilal anayecheza Tusker ya Kenya anaingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva anayecheza Difaa Al Jadid ya MoroccoDk 78, inaonekana mashambulizi ya Malawi kutoka upande wa mashariki ni hatari kwa afya ya lango la Tanzania Dk 70, Taifa Star

ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa maoni yake juu ya Baraza jipya la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko hii leo, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidiiUteuzi wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi mkubwa”, ameandika Zitto Kabwe. Leo Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa na vitengo vingi.

JPM Ateua Mawaziri Wapya, Lugola, Shonza Ndani, Maghembe, Kashililah Out

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri nchini huku akizigawanya baadhi ya wizara zikiwemo Wizara ya Kilimo na Mifugo, Nishati na Madini na kuongeza wizara mpya mbili na kufikisha jumla ya wizara 21. Katika Mabadiliko hayo, Mawaziri wawili na manaibu waziri wameongezwa. Aidha Rais Magufuli ametangaza mabadiliko na kuteua Katibu mpya wa Bunge huku akieleza kuwa aliyekuwa Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine. ORODHA. Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu: Naibu Waziri – Stella Alex Ikupa Wizara ya Mifugo na Uvuvi: Waziri – Luhaga Mpina, Naibu Waziri -Abdallah Hamisi Ulega. Wizara ya Maji na Umwagiliaj: Waziri- Mhandisi Isack Kamwelwe, Naibu Waziri – Jumaa Hamidu Aweso. Wizara ya Nishati: Waziri – Dk. Medard Kalemani, Naibu Waziri – Subira Khamis Mgalu. Wizara ya Madini: Waziri – Angellah Kairuki, Naibu Waziri -Stanslaus Haroon Nyongo. Wizara ya Maliasili na U

BREAKING NEWS: JERRY MURO AJIBU TUHUMA NZITO ZA CHADEMA, AMVAA MAZIMA LEMA

Image
      KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia aliwahi kuwa Msemaji wa klabu ya yanga, Jerry Muro ameibuka na kuwaponda viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akiwataka waache porojo na badala yake wajikite katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Muro amewataka viongozi wa Chadema wanaodai kuwa wanafuatiliwe na watu ili wauawe, waseme wanafuatiliwa na akina nani?“ Nimemsikia baadhi ya wabunge wa Chadema wakisema kuna watu wanawafuatilia, dada yangu kule Bunda (Ester Bulaya) akisema anafuatiliwa na watu waliovaa kininja, nani awafuatilie nyie? Kwani mmeiba makinikia?“Lema naye anasema wamefungua nati za gari lake, pia anadai akiwa kwenye mwendokasi aliona watu wanamfuatilia akaruka kwenye gari akamwachia usukani mkewe, hivi kweli gari lipo kwenye mwendokasi unarukaje kichakani? Acheni maigizo jamani…” Nani akutafute wewe Lema? Mbona husemi wakati ukiwa na nywele za rasta ulikuwa un