MKUU WA WILAYA YA MBULU AAGIZA KITUO CHA POLISI KUJENGWA HARAKA.




Mkuu Wa wilaya ya mbulu  chelestino s mofuga leo 09/10/2017 amekutana na wajumbe wa WDC  wa kata ya Eshkesh , kujadili maendeleo ya kituo cha polisi cha yaeda chini ambacho kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba 2017.

 Mkuu huyo amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi kuwachukua maelezo na  kuahidi kusimamia kikamilifu  michango ya wananchi ili kujenga kituo hicho. 

Mkuu wa wilaya aliunda tume kuchunguza matukio ya ujangili wa nyara za serikali, wizi wa mifugo na mauaji ya binadamu mnamo mwezi wa nne 2017, na moja ya mapendekezo ya uthibiti wa matukio ya uhalifu ni kujenga kituo cha polisi.

Wajumbe hao wamebainika kusuasua kusimamia michango licha ya wananchi kuunga mkono ujenzi huo. Mkuu wa wilaya ametoa siku 30 kukamilisha michango ya ujenI wa kituo cha polisi.

Comments

Popular posts from this blog