Hallelujah ya Diamond yaweka rekodi Kimataifa Yatikisa Uingereza
Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa
zinazohusiana na nyimbo zake kila kukicha. Baada ya kuachia wimbo wake
mpya ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha Morgan Heritage kuweka rekodi
kubwa ya kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 15, wimbo huo
umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra ya nchini
Uingereza.
Hallelujah’ umeshika namba moja katika Top 5 ya kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ . Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri nchini humo ikiwemo na kwenye kituo kingine cha Capital Xtra.
Comments
Post a Comment