Waziri wa afya afariki baada ya kukimbia

Slim Chaker aliteuliwa waziri wa afya mwezi uliopita

Waziri wa afya nchini Tunisia amefariki kutokana na mshutuko wa moyo baada ya kushiriki katika mbio za kuchangisha fedha za kusaidia kupambana na ugonjwa wa saratani.

Slim Chaker, 56, aliugua baada ya kukimbia mita 500, kufariki kwenye hospitali ya kijeshi, kwa mujibu wa wizara ya afya.

Waziri mkuu Youssef Chahed alisema kuwa amempoteza ndugu ambaye alikuwa akitoa huduma ya kibinadamu.

Wanawake waislamu nchini Tunisia waruhusiwa kuolewa na wanaume wasio waislamu

Mbio hizo ziliandaliwa kwenye mji wa pwani wa Nabeul siku ya Jumapili kuchangisha fedha za kujenga zahanati ya watoto ya kutibu ugonjwa wa saratani.

Bwana Chaker aliteuliwa kuwa waziri wa afya mwezi uliopita wakati wa mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri.

Comments

Popular posts from this blog