SHAMSA FORD AZIDI KUMSHUKIA ILALA MJINGA,AMPA MAKAVU LIVE

          UKITAKA kujua kichaa cha ‘Queen’ wa Bongo Muvi, Shamsa Ford, basi jaribu kuichokonoa ndoa yake, na hicho ndicho anachokifanya mtu mmoja aliyemfahamu kwa jina la Ilala Mjinga, ambaye kazi yake ni moja tu, kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuhusiana na ndoa yake na mumewe, Chid Mapenzi.

Kwa mujibu wa Shamsa ambaye siku chache nyuma alisema kuwa anamuona jini-mkatakamba anainyapianyapia ndoa yake, hatimaye mambo yakamfika shingoni na kuamua kushusha waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwataka wale wote ambao wanadhani atakuja kuachana na mumewe, basi wajue kwamba hiyo ni ndoto sawa na kusubiri embe dodo kwenye mti wa korosho! NA ISRI MOHAMED/GPL

Comments

Popular posts from this blog