CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI GIZA NENE, MADIWANI WALIOJIUZULU WATIMKIA CCM.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Chama
cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimalisha kwa
kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo
(CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo
la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA.
Akizungumza
wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa
CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua
kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano DR John Pombe Magufuli.
“Mimi
nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa
sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze
kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao nah ii ndio mikakati
yetu”alisemaRubeya
Rubeya aliwaambia
wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na
walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika
kufanya kazi za kukijenga chama cha mapinduzi.
“CCm
ni ndio chama tawala hivyo ondeeni hofu na mzidi kutupa maarifa
mliotoka nayo huko na kukisaidia chama hiki kuzidi kupata wananchama
wengi kutoka vyama vya upinzani na mkiwa CCM mtapikwa vizuri na kuwa
viongozi wazuri” alisema Rubeya
Aidha Rubeya aliwaambia
kuwa CCM hutoa madaraka kwa mtu yeyeto yule mwenye weredi katika nafasi
aliogombe hivyo huku hakuna kuteuana huku kuna nafasi za kugombea na
kuchaguliwa na wanachama cha mapinduzi tufati na kule mlikokuwa mnateuna
kwa maslai ya mtu mmoja.
Naye
katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Marko Mbaga aliwataja
wanachama waliohamia hamia chama hicho kutoka CHADEMA ni Baraka Kimata
aliyekuwa katibu mwenezi na Diwani wa kata ya Kitwiru,Theodora Mbata
aliyekuwa matroni wa wanawake kata ya Kitwiru, Erick Muyungo na Raymond
kimata aliyekuwa kiongozi wa redbrigad manispaa ya Iringa na katibu
mwenezi wa kata ya kitwiru.
“Hii
ni mwanzo tu watakuja wengi mno kwa kuwa CCm manispaa ya Iringa
wanachapa kazi hata kama halmashauri ipo kwa wapinzania lakini wao
wataendelea kufanya kazi kwa kutekeleza ilani ya chama chetu ili
kuwamaliza wapinzani wetu wote warudi kwenye chama tawala” alisema Mbaga
Edwin
bashir ni katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa alisema kuwa
sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa wananchi na wananchi waendelee kuwa
na Imani na chama cha mapinduzi ili waje kufanikiwa kulikomboa hili
jimbo ambao lipo upinzani.
“Mimi
najua vijana wengi muda sio mrefu wataanza kurudi nyumbani kwao kwenye
chama wananchokipenda na kuondokana na siasa za maji taka kwa kuwa CCM
ni tanuli za kuwahoka viongozi bora na sasa manispaa tutafanya kazi
kweli kweli na kuwamaliza wapinzani kwa nguvu zote” alisema Bashir
Baraka
Kimata,Theodora Mbata, Erick Muyungo na Raymond kimata walisema kuwa
watakitumikia ipasavyo chama cha mapinduzi kama walivyokuwa wanakitumika
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhakikisha CCM wanashinda
chaguzi zote watakazo kuwa wanashiriki katika manispaa ya iringa.
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalumu mkoa wa iringa kupitia chama cha
mapinduzi CCM Ritta Kabati aliwapongeza viongozi wote wapya
waliochaguliwa hivi karibuni na kuanza kufanya kazi inayoonekana machoni
mwa wakazi wa manispaa hiyo.
“Juzi
mmechaguliwa lakini kazi imeanza kwa kuwapata wananchama wapya
wanaotoka upinzani kurudi CCM hiyo sio kazi ndogo kwa kweli hiyo ni kazi
kubwa sana ambayo mmeanza nao nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa
mnachokifanya kuhakikisha tunapata wanachama wengi kutoka upinzani”
alisema Kabati
Comments
Post a Comment