FT: TANZANIA 1-1 MALAWI kKUTOKA UWANJA WA UHURU

Kikosi cha timu ya Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Malawi leo Uwanja wa Uhuru Dar.
Kikosi cha timu ya Malawi.
MPIRA UMEKWISHA
Dk 90+4 Samatta yuko chini anatibiwa baada ya kugongana na beki wa Malawi wakati akijaribu kufunga, wote wametolewa nje kutibiwa
Dk 90+2 Muzamiru analambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu ya pili kwa Taifa Stars
Dk 90 nafasi nyingine ya Taifa, lakini kipa wa Malawi anaokoa
Dk 90 nafasi nyingine ya Taifa, lakini kipa wa Malawi anaokoa
Dk 88 Mbaraka Yusuf anapoteza nafasi akiwa yeye na lango, kazi nzuri ya Samatta ameshindwa kuitumia
Dk 85, Nyoni amepewa kadi nyekundu, mwamuzi anamtuhumu kumpiga mwenzake kiwiko lakini mchezaji huyo wa Malawi, hakuadhibiwa kwa kuwa alimvamia Nyoni

Dk 83 Abdul Hilal anayecheza Tusker ya Kenya anaingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva anayecheza Difaa Al Jadid ya MoroccoDk 78, inaonekana mashambulizi ya Malawi kutoka upande wa mashariki ni hatari kwa afya ya lango la Tanzania
Dk 70, Taifa Stars wanaonekana angalau kufanya mashambulizi makali, mkwaju wa kichwa wa Samatta umegonga mwamba

Taifa Stars wamemtoa Shiza Kichuya na nafasi yake imechukuliwa na Ibrahim Ajibu MigombaDk 60 sasa, kidogo Malawi wanaonekana kuchanganyikiwa na kuanza kucheza kindavaDk 57 Taifa Stars inapata bao safi kupitia kichwa kilichopigwa na Saimon Msuva
Dk 56 sasa, hakuna matumaini makubwa ingawa Stars wanazidi kupeleka mashambulizi kadhaa. Mabeki wa Malawi wanaonekana ni wazuri zaidi wa mipira ya juu, huenda itakuwa vizuri Stars wakijaribu kupita chini.
Dk 47 sasa, kipindi cha pili kimeanza, Taifa Stars wakiongozwa na nahodha Samatta wanaonekana wamepania kusawazisha, lakini Malawi wako makini sana.
MAPUMZIKO:
Hadi mapumziko, Taifa Stars imekwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Malawi.
Katika mechi hiyo ya kirafiki bao la Malawi, limefungwa na Ngambi Robert katika dakika ya 35.

PICHA: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments

Popular posts from this blog