Posts

Majibu ya Ndugai kwa Lema kuhusu lissu

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo. "Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai Pia Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge. "Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyop

Breaking News: Mahakama ya Kisutu yamuachia huru Yusuph Manji

Image
KISUTU: Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake. Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali. Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

JESHI LA POLISI DODOMA LASIKITISHWA NA KITENDO CHA DEREVA WA TUNDU LISSU KUTOFIKA POLISI

Image
        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake. Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo. Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo. Wamiliki wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia gari hizo,” amesema.Hata hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi. Tunasikia yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa tukio hilo.”

“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani yetu”: Waziri Mkuu

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ipo salama na imara na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria. Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Septemba 13, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam. “Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu. Nawaomba wananchi muwe makini na muendelee kuidumisha amani yetu.” Amesema kwa sasa Serikali ipo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi, rushwa, biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na wahujumu uchumi. Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano. Amesema mbali ya kuimarisha amani nchini, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija. Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribis

Lusekelo: Tusimtumie Lissu kupata umaarufu

Image
 Mchungaji Lusekelo ameandika ujumbe huo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mbona watu hao hawakuonekana kulaani mauaji ya Kibiti au kuitisha maombezi baada ya watu Kibiti kuuawa. "Tusitumie tatizo la ndugu yetu Tundu lissu kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini, mtu yeyote ambaye anatumia tukio hili kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini namfananisha na wale wahuni ambao basi likianguka anaenda kuchukua simu kwanza, ni jambo ovu sana wewe unakuwa ni sehemu ya watu walio mpiga risasi Tundu lissu. Mwenzako anaumwa wewe unatumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu wa kidini au wakisiasa ni jambo baya sana, mbona sikusikia wakilaani mauaji ya kibiti au kuitisha maombezi watu wakibiti walipo uwawa, mbona hawaja laani utekaji na mauaji ya watoto Arusha hata wa Marekani (umoja wa ulaya) sikusikia wanalaani mauaji ya kibiti" aliandika Mzee wa Upako Aidha Mchungaji huyo amesema kuwa yeye anaamini watu hao wanatumia matatizo ya Tundu Lissu

Man U, PSG, Barcelona na Chelsea Zaua Ligi ya Mabingwa Ulaya

Image
Mchezo ukiendelea wa Ligi ya Mabingwa Ulaya  Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Manchester na Basel. MANCHESTER United imerejea kwa nguvu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Basel, kama ilivyo kwa wababe wa Hispania, Barcelona waliopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus. Msimu wa 2017/18 wa michuano hiyo hatua ya makundi ulifunguliwa usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na mechi nyingi kwenye viwanja tofauti huu vigogo wengi wakiibuka na ushindi. Fellaini akishangilia baada ya kutupia bao la kwanza kwa Man Utd. MANCHESTER UNITED 3- 0 BASEL Ikicheza kwenye uwanja wake wa Old Traff ord, United ilipata ushindi huo muhimu katika Kundi A, mpira ukiwekwa wavuni na Marouane Fellaini dakika ya 35 na Romelu Lukaku dakika ya 53, mabao yote yakifungwa kwa kichwa huku Marcus Rashford akitokea benchi na kuifungia timu yake bao la tatu. Katika mchezo huo, kiungo wa United, Paul Pogba aliyekuwa nahodha wa kikosi chake aliumia da

BREAKING NEWZ: Mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali

Image
Taarifa zilizoifikia muda huu kuhusiana na mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali ya gari akiwa katikati ya  Nyasamba na Bubiki mkoani  Shinyanga . MC Pilipili amepata ajali akiwa kwenye garia aina ya Prado na kukimbizwa hospitali, kwa matukio na habari zaidi zinafuatilia kwa ukaribu ili kuweza kukuletea habaria kamili.

ANGALI PICHA WEMA SEPETU AKIWA MAHAKAMANI KWENYE KESI YAKE,SHAHIDI AFICHUA ALIPOIKUTA BANGI

Image
                    Wema Sepetu akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu MKaziKisutu Dar. Wema na mama yake wakielekea kupanda gari. SHAHIDI upande wa serikali kesi ya Wema Sepetu kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya amesema msokoto wa bangi ulikutwa ukiwa kabatini jikoni kwake. Hayo yamesemwa na ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy akimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula. Inspekta Willy anakumbuka Februari 4, mwaka huu aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa              Wema Sepetu ambapo aliongozana na maofisa wenzake hadi nyumbani anakoishi huko Ununio jijini Dar es Salaam. Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta mfanyakazi wake wa ndani wa kike ambaye walimuomba waonane na mjumbe wa shina wa maeneo hayo ambapo baada ya kufanikwa kumwona walimweleza shida yao na kuanza kazi ya uchunguzi ili kutafuta dawa za kule

JPM Amjulia Hali Meja Jenerali Mstaafu Aliyejeruhiwa kwa Risasi

Image
Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo. RAIS John  Magufuli leo Jumanne ametembelea Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli akisalimiana na mtoto. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana  mchana na kisha kupelekwa katika hospitali ya jeshi Lugalo kwa matibabu. Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo. Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais Magufuli kuwa Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitika sana kama haoni jeshi heshima ya Bunge inavyoshuka. Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni. Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala asingehaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha. "Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu k

HAMISO MOBETTO AFUNGWA MDOMO,KISA KUZAA NA MSANII

Image
             Hamisa Mobetto. MAMA mzazi wa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto anayedaiwa kuzaa na msanii wa Bongo Flava, amecharuka akisema kuwa, japokuwa mtoto wake huyo anapigwa vijembe, lakini kamwe hawatamsikia akisema kwa sababu amemwambia afunge mdomo. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mama Mobetto alisema kuwa, yeye kama mama anasikia uchungu kuona mwanaye huyo anavyosengenywa, lakini kwa busara amemtaka kutofungua mdomo kujibizana na mtu yeyote kuhusiana na ishu hiyo. Hamisa hatafungua mdomo kuzungumza chochote kuhusiana na mtoto wake na siyo mjinga kunyamaza, ila tu hatutaki malumbano na mtu,” alisema mama Mobetto.

Katibu Mkuu Chadema Ahojiwa Kuhusu ‘Watu Wasiojulikana’

Image
Dk Vincent Mashinji. KATIBU Mkuu wa Chadema , Dk Vincent Mashinji amesema polisi wamemhoji wakitaka kujua kuhusu kauli zake za watu wasiojulikana kama anaweza kuwatambua. “Watu wasiojulikana ambao tulikuwa tunawaongelea ni kwamba, imezoeleka kwa polisi kunapokuwa na tukio kubwa wanasema watu wasiojulikana, kwa hiyo lengo langu lilikuwa ni kuita wananchi  kurudi kwenye Polisi Jamii ili kuondokana na hili la watu wasiojulikana,” alisema Dk Mashinji. Katibu mkuu huyo wa Chadema, leo Jumatatu ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini hapa. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene ilisema Dk Mashinji aliambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho. “Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (

Breaking News: Watu Wasiojulikana Wavamia Ofisi za Wakili wa Manji

Image
Polisi wakiwa eneo la tukio. Ofisi ya mawakili ya Prime Attorneys imevamiwa usiku wa manane na watu wasiojulikana ambao wameiba kasiki lenye fedha na nyaraka. Mmoja wa mawakili katika ofisi hiyo,  Hudson Ndusyepo amesema ofisi yao imevunjwa na tayari ameenda polisi kutoa taarifa. Ndusyepo ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaomtetea mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi, amesema kabla ya wizi huo, waliohusika walimfunga mlinzi kwa kamba.   Milango ilivyovunjwa. Kampuni ya Prime Attorneys katika tovuti yake inaeleza ilianzishwa mwaka 2010. Ofisi za kampuni hiyo zipo Jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam. Ofisi hizo zipo kwenye jengo la ghorofa tano lililopo jirani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala. Leo Asubuhi barabara ya kuingia eneo hilo ilifungwa kwa muda na polisi ambao walitumia magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa  utepe wa rangi ya njano. Wakili

Vyakula Vinavyoliwa na Mgonjwa wa Vidonda Vya Tumbo

Image
LEO tutaangazia vyakula tiba kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo. Tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa wa vidonda vya tumbo (Ulcers) ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao. Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa huo unapaswa kujiepusha kula vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi. Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha. Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivyo kwani huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa. Kuna uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa

Je unajua vyoo vya kukaa vina madhara kiafya kwa watumiaji

Image
Nyumba haiwezi kuwa kamili bila kuwa na huduma hiyo ya choo, Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa choo, lakini si kila nyumba iliyo na choo au hata zile ambazo zina huduma hiyo, basi vyoo ni vibovu, havina hadhi. Zipo aina mbalimbali za vyoo kwa matumizi ya binadamu katika maisha yake ya kawaida. Vyoo vina matumizi mengi ingawa  bado  watu wengi  hasa katika nchi maskini na zinazoendelea ikiwamo Afrika wanatumia choo cha kuchuchumaa wakati wa kujisaidia, lakini mijini na katika nchi zilizoendelea, wao hutumia vyoo vya kukaa. Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’. Mgunduzi wa vyoo vya aina hii, Thomas Crapper anasema kwa mtazamo wake aliona kukaa wakati wa kujisaidia ni utambulisho wa ustaarabu na maendeleo. Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa k

ANGALIA PICHA YA KWANZA MADAKTARI WALIOKOA MAISHA YA TUNDU LISSU

Image
                       Timu ya Madaktari waliookoa uhai wa Mh Lissu kwa huduma ya dharula Mjini Dodoma wakiwa chini ya Dr. Mpoki(Katibu Mkuu W/Afya), Dr. Mponda (Orthopaedic), Dr. Samwel (Orthopaedic),na Dr. frank.Mh Lissu tayari ameondoka katika ardhi ya Tanzania na kwenda Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi akiambatana na mkewe kipenzi wakili msomi Alicia Lissu sambamba na Mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe, na Mh. Peter Misigwa.

Kanisa la Askofu Gwajima labomolewa

Image
Dar es Salaam. Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Mbezi Inn linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima limebomolewa. Nyumba hiyo ya ibada ambayo pia ilikuwa ikitumika kama kituo cha maombezi imebomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads). Imeelezwa kanisa hilo limejengwa ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro ya mita 121.5. Kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo, pia limekuwa likitumika  kama kituo cha kufundishia wachungaji limebomolewa jana jioni hali iliyosababisha waumini wa Kanisa hilo kusalia nje. Mwananchi imefika katika kanisa hilo na kukuta  vitu vikiwa nje na baadhi ya waumini wakiendelea  na maombi nje. Mmoja wa waumini ambaye hakutaka kujitambulisha kwa madai si msemaji, amesema kanisa leo limebomolewa lakini injili inaendelea kuhubiriwa kama kawaida . "Tunaendelea na huduma na kesho tutakuwa na ibada itakayoanza saa kumi jioni "amesema. Muumini mwingine pia amesema hali ilikuwa mbaya jana wakati kanisa hilo linabomolewa kwani wali

Kauli ya Rais Magufuli Baada ya Kupata Taarifa za Lissu

Image
RAIS John Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake kutokana na kushambuliwa kwa kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema). “Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria,” amesema Rais Magufuli. Stori zinazo husiana na ulizosoma

BREAKING: Tundu Lissu Apigwa Risasi

Image
MBUNGE wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi zinazodaiwa kuwa tano. Tukio hilo linadaiwa kutokea leo akiwa nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma ambapo watu hao walimvamia akiwa kwenye gari kisha kumpiga risasi za miguuni na tumboni. Imeelezwa kuwa alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.  Dereva wake akiwa ameshika nguo na viatu vya Tundu Lissu Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana. Gari la Mbunge Lissu likionekana na baadhi ya matundu zilipopigwa Risasi  Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji. "Hli ya Tundu Lisu ni mbaya Sana

Kutajwa Sakata la Madini… Waziri Simbachawene, Ngonyani Wajiuzulu

Image
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene. WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wameandika barua za kujiuzulu nyadhifa hizo ili kupisha uchunguzi baada ya kutajwa kuhusika kwa ubadhilifu kwenye Ripoti za Uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite. Uamuzi a viongozi hao umekuja ikiwa ni dakika chache baada ya Rais Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo Rais aliwataka viongozi wote wa serikali walioko madarakani na wametajwa kuhusika kwenye kashfa hizo waachie ngazi ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya usalama. Kwa upande wake, akiongea na Mwananchi leo Alhamisi mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na sasa anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo. Naibu Waziri w