JPM Amjulia Hali Meja Jenerali Mstaafu Aliyejeruhiwa kwa Risasi

Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo.
RAIS John  Magufuli leo Jumanne ametembelea Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli akisalimiana na mtoto.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana  mchana na kisha kupelekwa katika hospitali ya jeshi Lugalo kwa matibabu.

Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo.
Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais Magufuli kuwa Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.
Rais Magufuli akimjulia mmoja wa wagonjwa wliolazwa hospitalini hapo.
Katika taarifa hiyo ya Msigwa ameeleza kuwa  Mritaba amemshukuru Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.
Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo.
Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo pia ametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu.

Comments

Popular posts from this blog