Majibu ya Ndugai kwa Lema kuhusu lissu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo.

"Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai

Pia Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge.

"Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyopelekwa Lissu", amesema Spika Ndugai.

Pamoja na hayo Spika Ndugai amesema anamsamehe Godbless Lema na kuwataka watu kumsamehe kwani hajui alitendalo
Hapo jana mbunge wa Arusha Godbless Lema alimlaumu Spika Ndugai kuwa anashindwa kutetea kiti chake, kwa kuzidi kuwakandamiza wabunge wa upinzani hususan suala la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.

Comments

Popular posts from this blog