BREAKING: Tundu Lissu Apigwa Risasi

MBUNGE wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi zinazodaiwa kuwa tano.
Tukio hilo linadaiwa kutokea leo akiwa nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma ambapo watu hao walimvamia akiwa kwenye gari kisha kumpiga risasi za miguuni na tumboni. Imeelezwa kuwa alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.
 Dereva wake akiwa ameshika nguo na viatu vya Tundu Lissu

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.

Gari la Mbunge Lissu likionekana na baadhi ya matundu zilipopigwa Risasi 
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.

"Hli ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa"- Ameeleza Freeman Mbowe
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa ajili ya kufahamu taarifa zaidi

Comments

Popular posts from this blog