ANGALI PICHA WEMA SEPETU AKIWA MAHAKAMANI KWENYE KESI YAKE,SHAHIDI AFICHUA ALIPOIKUTA BANGI
Wema Sepetu akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu MKaziKisutu Dar. Wema na mama yake wakielekea kupanda gari. SHAHIDI upande wa serikali kesi ya Wema Sepetu kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya amesema msokoto wa bangi ulikutwa ukiwa kabatini jikoni kwake. Hayo yamesemwa na ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy akimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula. Inspekta Willy anakumbuka Februari 4, mwaka huu aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema Sepetu ambapo aliongozana na maofisa wenzake hadi nyumbani anakoishi huko Ununio jijini Dar es Salaam. Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta mfanyakazi wake wa ndani wa kike ambaye walimuomba waonane na mjumbe wa shina wa maeneo hayo ambapo baada ya kufanikwa kumwona walimweleza shida yao na kuanza kazi ya uchunguzi ili kutafuta dawa za kule