
Zarina Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’ . BAADA
ya maneno mengi kusemwa Bongo kufuatia madai ya bwana’ke kuzaa na
mwanamitindo mwenye jina kubwa, Hamisa Hassan Mobetto, mwanamama
mjasiriamali mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Zarina Hassan Tiale
‘Zari The Boss Lady’ anadaiwa kuendelea kuliamsha dude baada ya kutinga
Bongo na kuanza kudodosa ili kupata ukweli wa ishu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni makini, awali Zari alitinga
Bongo mapema wiki iliyopita na kupigwa chabo na ‘wadakuz’ AKIWA KATakiwa
nyumbani kwa jamaa huyo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva huko Madale
jijini Dar. Akiwa katika pozi. Ilidaiwa kwamba, hata hivyo, hakukaa sana
kwani aliondoka kwenda kwenye kumbukumbu ya siku 40 za kifo cha mama
yake, Halima Hassan nchini Uganda kabla ya kurejea Bongo wikiendi
iliyopita.

Kwa taarifa yenu Zari amejaa tele Bongo na lengo lake ni
kuchimba na kupata ukweli juu ya madai ya Hamisa kuzaa na
bwana’ke.Unajua akiwa Sauz hapati mtiririko mzuri wa kinachoendelea
Bongo ndiyo maana ameona aje kuchimba mwenyewe ili ajue mbivu na mbichi
na ajue nini cha kufanya,” kilidai chanzo hicho.Kilizidi kutiririsha
madai kwamba, endapo Zari atabaini ukweli kuhusu mzazi mwenzie huyo
kuzaa na Hamisa, basi kuna uamuzi mzito atachukua. Hamisa Hassan
Mobetto.

Hata hivyo, gazeti hili lilizungumza na mmoja wa memba
wa familia ya msanii huyo ambaye amezaa na Zari watoto wawili ambaye
alithibitisha uwepo wa mwanamama huyo, lakini akaomba hifadhi ya
jina.Wewe jua tu kwamba, yupo, amejaa tele. Kuhusu hayo mambo yake na
Hamisa mimi sijui maana sijamsikia akilizungumzia. So labda anafanya
kimyakimya,” alisema memba huyo wa familia.
Kwa upande wake Hamisa, habari zilizolifikia Ijumaa Wikienda katika
dakika za lala salama kuelekea kiwandani zilidokeza kuwa, mrembo huyo
kwa sasa ameamua kumuhudumia mwanaye mwenyewe na kwamba, maandalizi ya
shughuli ya 40 ya kumtoa mtoto wake huyo yamepamba moto. Stori: Imelda
Mtema | Ijumaa Wikienda
Comments
Post a Comment