Posts

ADAM MALIMA ATISHIWA BUNDUKI NA POLISI

Image
TAHARUKI imeibuka mchana huu maeneo ya  Masaki karibu na Double Tree Hotel baada ya askari polisi mmoja kufyatua risasi hewani kutokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa mzozo kati ya polisi na mbunge wa zamani wa Mkuranga, Pwani, Adam Kighoma Ali Malim. Taarifa zimeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na polisi walipojaribu kukamata gari lililokuwa limeegeshwa barabarani. Inasemekana gari lilikuwa la mwanaye Kighoma Malima aliyekuwa eneo hilo kwa shughuli zake binafsi ambapo ofisa wa Majembe alivamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndipo wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakizania ni jambazi. Polisi aliingilia kati na katika majibizano ya maneno na Malima, ndipo askari mmoja akafyatua risasi kadhaa hewani hali iliyozua taharuki kubwa eneo hilo. Mtandao wa Global Publishers umefanya jitihada za kumtafuta Malima kwa njia ya simu lakini simu zake

Mwigulu Nchemba: Bado Hatuna Sheria ya Kuthibiti Shisha

Image
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba bungeni leo amesema serikali bado haina sheria ya kuthibiti matumizi ya kilevi aina ya shisha ila lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku biashara hiyo na kutaka agizo hilo lifuatwe na kila mtu. Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali bungeni kuhusu matumizi ya kilevi hicho cha shisha ambacho bado katika baadhi ya maeneo kimeendelea kutumika na kuleta athari kwa watumiaji. “Ni kweli serikali baada ya kuona matumizi ya kilevi cha Shisha yanaleta athari kwa binadamu, serikali imeanza kuweka sheria za kuthibiti matumizi ya shisha, usambazaji wa shisha na uagizaji wa kilevi hicho, lakini wakati tunasubiri sheria hizo tunatambua kuwa lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku matumizi ya kilevi cha shisha ambalo utekelezaji wake ulianza mikoani kama Dar es Salaam, Mbeya, Iringa na mikoa mingine imeendelea kuitikia. Kwa hiyo maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu yanafanyiwa kazi bila kupunguza hata

Mwanafunzi Kukishitaki Chuo Kikuu cha UDSM

Image
Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Alphonce Lusako, amewasilisha maombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, aruhusiwe kukishtaki chuo hicho kwa kumkatisha masomo. Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya sheria alifukuzwa baada ya kufutiwa usajili Januari 26, pamoja na mambo mengine akidaiwa kusajiliwa kwa makosa kwasababu aliwahi kufukuzwa chuoni hapo. Lusako anayewakilishwa na Wakili Jebra Kambole anaiomba Mahakama impe kibali cha kuishtaki UDSM na itoe amri ya kuzuia uamuzi wa kumfutia usajili. Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa Mei 23 na Jaji Pellagia Khaday. Lusako alijiunga na UDSM kwa mara ya kwanza mwaka 2009 akiwa amedahiliwa kusoma Shahada ya Biashara katika Uhasibu. Hii ni mara ya pili kwa Lusako kufukuzwa chuoni hapo, mara ya kwanza ni Desemba 13, 2011, pamoja na wenzake kadhaa, akiwa mwaka wa tatu walifukuzwa na kufutwa katika mfumo wa elimu nchini wakidaiwa kuratibu mgomo wa wanafunzi UDSM. Hata hivyo

RAIS DKT. MAGUFULI AIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU CDA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilikiza viongozi mbalimbali waliokuwa wakichangia mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. m. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sh

MBUNGE LEMA ADAI UPINZANI TANZANIA NI KAZI SANA

Image
  Mbunge Godbless Lema amedai kuwa mpinzani wa siasa za bongo ni kazi ngumu sana, Mh Lema amesema hayo baada ya baaadhi ya watu kumdhihaki alipotoa shukrani zake kwa Mbunge Lazaro Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali ya basi la Lucky Vicent. Jana baada ya Mbunge Godbless Lema kumshukuru Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu kuna kundi la watu liliibuka na kuanza kutoa maneno ya dhihaka kwa Lema huku wengine wakipongeza na kusema ni jambo la kheri kwa mbunge huyo kutambua kazi iliyofanywa na Nyalandu, lakini baada ya mijadala hiyo kuzidi kuwa mikuba aliibuka Mh. Lema na kutoa kauli hii kumjibu mtu mmoja ambaye alikuwa akimdhihaki.  "Kuwa mpinzani wa siasa Tanzania ni kazi ngumu sana, ila hatukati tamaa kwa sababu upendo wetu ni mkuu kuliko dhihaka. Mungu akubariki"   aliandika Godbless Lema 

CCM yawasimamisha viongozi wengine Arusha

Image
Monday, May 15, 2017 Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Arusha  kimewasimamisha viongozi wa kata mbili kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwepo kushindwa kuratibu vyema chaguzi ndani ya chama hicho. Wiki iliyopita Katibu  wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole aliwasimamisha viongozi zaidi ya 30 wa kata tano, baada ya kubainika wameshindwa kusimamia majukumu yao. Chama hicho kimeendelea na hatua hiyo, ambapo leo (Jumatatu) viongozi wa kata ya Ngarenaro na Kaloleli wamesimamishwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa chama hicho, kujiimarisha katika jiji la Arusha, baada ya kupoteza mvuto ambao ulisababisha kushindwa katika uchaguzi uliopita. Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, wilaya ya Arusha ,Gasper Kishimbua amesema  CCM imechukuwa uamuzi huo, ili kuendelea kujiimarisha chama hicho. Kishimbua amewataja waliosimamishwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kata ya Kaloleni, Amin Ngawala na Katibu wake, Regina Kessy. Katika Kata ya Ngarenaro, waliosimamishwa ni Mwenyekiti, Ally Mw

BREAKING: “Hans Pope amefuta uamuzi wa kujiuzulu uongozi Simba” – Haji Manara

Image
Baada ya kuripotiwa taarifa za kujiuzulu kwa Hans Pope Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, leo Jumatatu May 15, 2017 ripoti mpya kutoka kwa Afisa Habari wa club hiyo Haji Manara kutoka kwenye Instagram yake ameandika kuwa kiongozi huyo amefuta uamuzi wake. Kupitia Instagram Haji Manara ameandika >>>  Rasmi Hanspope arejea kundini, afuta uamuzi wake wa kujiuzulu, na ndio maana fans wetu nawaomba mtulie, hakuna kitakachoharibika, ni upepo mbaya ulipita na sasa umetulia, Karibu tena kamanda Pope<<< – Manara

Gigy Amchefua Wema Ukumbini

Image
Stori: Waandishi Wetu | IJUMAA WIKIENDA | D AR ES SALAAM Muuza nyago kwenye video za nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kumtia hasira na kumchefua staa wa sinema za za Kibongo, Wema Isaac Sepetu baada ya kukutana ukumbini kwenye bethidei ya meneja wa wasanii wa muziki. Ubuyu wa motomoto ulidai kuwa, baada ya kukutana, Gigy alidaiwa kucheza muziki kihasarahasara na mmoja wa ‘mazilipendwa’ wa Wema, jambo ambalo mlimbwende huyo hakupendezwa nalo. Ishu hiyo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel uliopo Posta jijini Dar ambapo mastaa kibao walikuwa wageni waalikwa kwenye shughuli hiyo iliyotawaliwa na mavazi ya kizamani. Wema Sepetu Kwa mujibu wa shushushu wa Wikienda aliyekuwa ndani ya shughuli hiyo, awali Wema alionekana mwenye bashasha tele akiwa na wapambe wake, lakini Gigy alipoanza makeke yake ndipo bibie huyo akapoa kama maji ya mtungi. “Mwanzoni Wema hakuwa na tatizo kabisa na Gigy, lakini baa

KIMENUKA MSIMBAZI, MO AIDAI SIMBA BILIONI ZAKE.

Image
Siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa, mdau wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘MO’ anataka kulipwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 za Tanzania kutokana na viongozi wa Simba kukiuka makubaliano Mei 12, 2017, uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu Bw. Evans Aveva, ulisaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni. MO anataka kulipwa pesa zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji wa Simba tangu mwaka jana baada ya kubaini kuwa Simba imeingia mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha. MO kawaandikia Simba ‘demand note’ kwa kua wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe pesa kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya. Simba ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhu

BREAKING: KATIBU CCM AUAWA USIKU WA KUAMKIA LEO

Image
Kibiti.   Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani hapa, Alife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo (Jumapili)  katika Kijiji cha Nyambunda. Amesema Mtulia aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga. Kamanda amesema mwili wa marehemu umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi. Mauaji ya askari Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa yakifanyika mara kwa mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani. Jumanne wiki hii akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Mafia. Utaitwa mkoa wa kipolisi Rufiji. Credit : Muungwana

Wanachuo Wengi kukosa tena mikopo

Image
BUNGE limeishauri serikali kuongeza bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) baada ya kubaini wanafunzi wengi watakosa fedha hizo mwakani kutokana na bajeti ndogo iliyotengwa. Ushauri huo ulitolewa bungeni mjini hapa juzi na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ilipokuwa ikiwasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi na makadirio ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha. Akiwasilisha taarifa hiyo, mjumbe wa kamati hiyo, Hussein Bashe, alisema wamebaini wanafunzi wengi watakosa mikopo mwaka ujao wa fedha licha ya kuwa na ufaulu mzuri. Alisema mwaka huu wa fedha wanafunzi 48,502 walijaza fomu kwa ukamilifu lakini 25,555 tu ndiyo walipata mikopo na hivyo kuacha wengine 22,947 wakiwa hawana mikopo kutokana na bajeti iliyotengwa ya Sh. bilioni 427.5 kutotosheleza mahitaji. Bashe ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), alisema mwaka ujao wa fedha HESLB

MCHUNGAJI ALIWA NA MAMBA WATATU AKIJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU NCHINI ZIMBABWE

Image
Mchungaji wa kijiji kimoja huko zimbabwe Pastor Jonathan Mthethwa ametafunwa vizuri na mamba watatu alipokuwa akijitutumua kutembea juu ya maji Kama yesu katika mto MPUMALANGA au kwa jina maarufu MTO MAMBA kutokana na wingi wa mamba katika mto huo. Alikuwa anafanya majaribio ya imani(DEMO) aliyowafundisha waumini wake kanisani.... Shemasi aliyehojiwa anashangaa kwa nini aliliwa maana kabla alifunga na kuomba wiki nzima... Mashuhuda wanasema alitembea ndani ya maji kama mita 30, alipotaka kuanza kupanda ili aanze kutembea juu ya uso wa maji ndipo yalitokea mamamba makubwa matatu na kumtafuta na kumkatata vipande huku mwili wote ukiishia kwenye matumbo ya watafunaji hao... Waumini Muwe makini na Wachungaji wenu, Leo kaenda yeye kesho anaweza kuibuka mwingine TZ akawaambia kanisa zima litembee juu ya mto ruvu ile sehemu yenye mamba na viboko wengi kama mazoezi ya Imani. Au kama mafunzo ya vitendo baada ya kufundishwa Theory/Nadharia za kiimani kanisani.. Imani

FAHAMU UKWELI JUU YA VITA VYA KARANSEBES AMBAVYO ZAIDI YA WANAJESHI 10000 WALIUANA

Image
Unaweza kudhani ni hadithi ya kutunga lakini hii kweli ilitokea! Vita ya Karansebes, ni miongoni mwa matukio yaliyoushangaza sana ulimwengu baada ya wanajeshi wa jeshi moja la Austria, kushambuliana wenyewe kwa wenyewe na kusababisha wanajeshi zaidi ya 10,000 kupoteza maisha. Ilikuwaje? Usiku wa Septemba 17, 1788, wanajeshi zaidi ya 100,000 wa Jeshi la Austria lililokuwa linaundwa na makabila mbalimbali, walikuwa wameweka kambi katika Mji wa Karansebes (Romania ya sasa) wakijiandaa kuvamia Himaya ya Ottoman (Uturuki ya sasa). Ili kurahisisha uvamizi, wanajeshi waligawana katika makundi, wengine wakaenda upande mmoja na wengine upande mwingine. Wakati wakijiandaa kufanya shambulio, kukatokea kutoelewana kati yao, wakaanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe kimakosa wakidhani wanawapiga wanajeshi wa Ottoman. CHANZO CHAKE KINASHANGAZA Inaelezwa kuwa kundi moja kati ya yale mawili, lilivuka Mto Timis na kuingia Mji wa Hussar uliokuwa ngome ya wanajeshi washiri

Tamasha la Dar Bodaboda Superstar Lafanyika

Image
Baadhi ya washiriki wakiwa katika michuano ya kuendesha bodaboda. Bodaboda iliyokuwa ikishindaniwa na waendesha Pikipiki. Baadhi ya wananchi wakifuatilia michuano hiyo. Mkurugenzi Mkazi wa International Republican Institute(IRI),Robina Namusisi akizungumza na Global TV Online. Burudani zikiendelea. MAKAMPUNI ya JP Decaux pamoja na International Republican Institute (IRI) zilizokuwa zimeandaa Tamasha la Waendesha Pikipiki leo limefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers Jijini Dar es Salaam. Kati ya washiriki wa tamasha hilo la bodaboda mmoja alijinyakulia pikipiki baada ya kuwashinda washiriki wengine kutokana na vigezo vya mashindano hayo kuvikidhi. Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JP Decaux, Shaban Makugaya alisema kuwa lengo la tamasha hilo lilikuwa ni kuweka uamsho, msisitizo na kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki na abiria kwa madhumuni la kuzingatia sheria za us

Fainali za U-17 Afrika, kuanza Leo Gabon

Image
FAINALI za 12 za Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinatarajiwa kuanza leo mjini Franceville, Gabon hadi Mei 28, mwaka huu itakapofikia tamati. Mechi mbili za Kundi A zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Franceville kuanzia Saa 10:00 jioni kati ya wenyeji Gabon dhidi ya Guinea na baadaye Saa 1:00 usiku kati ya Cameroon na Ghana. Mechi za Kundi B zitaanza kesho, kwa michezo miwili pia kuchezwa Uwanja wa Port-Gentil, ya kwanza Saa 9:00 Alasiri kati ya mabingwa watetezi, Mali na Tanzania wanaoshiriki kwa mara ya kwanza kabisa michuano hiyo na wa pili utazikutanisha Angola na Niger kuanzian Saa 12:00 jioni. Awali michuano hiyo ilikuwa ifanyike Madagascar kuanzia Aprili 2 hadi 16, mwaka huu lakini Kamati Kuu ya CAF chini ya rais wake wa zamani, Mcameroon Issa Hayatou ikaipokonya uenyeji nchi hiyo Januari mwaka huu kwa madai Kamati ya Ukaguzi iligundua mapungufu makubwa. Ingawa hiyo ilih

Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Image
Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa. Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa. Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum. Spinachi Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele. Chai ya Kijani (Green tea) Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.  Mafuta ya samaki  Zipo aina nyingi

Kauli ya Rais Mstaafu Mkapa Kuhusu Serikali Kubana Uhuru wa Habari

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa amevikosoa vyombo vya habari barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahari kwa kile alichosema vingi vimejikita katika kuripoti habari za kisiasa na matukio ya nani kafanya nini au kawa nani, badala ya kuripoti habari za uchumi za kuwasaidia wananchi. Mzee Mkapa aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahijiano na na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) ya nchini Ujerumani ambapo alisema kwenye vyombo vya habari vya Afrika kuna upungufu mkubwa wa wa habari za uchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina. “Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba habari nyingi zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.” “Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea maendeleo. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige

Fahamu Aina 61 Za Ubanaji Wa Nywele

Image