CCM yawasimamisha viongozi wengine Arusha

Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Arusha  kimewasimamisha viongozi wa kata mbili kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwepo kushindwa kuratibu vyema chaguzi ndani ya chama hicho.

Wiki iliyopita Katibu  wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole aliwasimamisha viongozi zaidi ya 30 wa kata tano, baada ya kubainika wameshindwa kusimamia majukumu yao.

Chama hicho kimeendelea na hatua hiyo, ambapo leo (Jumatatu) viongozi wa kata ya Ngarenaro na Kaloleli wamesimamishwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa chama hicho, kujiimarisha katika jiji la Arusha, baada ya kupoteza mvuto ambao ulisababisha kushindwa katika uchaguzi uliopita.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, wilaya ya Arusha ,Gasper Kishimbua amesema  CCM imechukuwa uamuzi huo, ili kuendelea kujiimarisha chama hicho.

Kishimbua amewataja waliosimamishwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kata ya Kaloleni, Amin Ngawala na Katibu wake, Regina Kessy.

Katika Kata ya Ngarenaro, waliosimamishwa ni Mwenyekiti, Ally Mwelesi Katibu kata,  Chrisanta Mwinyimvua,  Yusuph Sharifu, Katibu uchumi na fedha Emmanuel Senyangwe.

Comments

Popular posts from this blog