KIMENUKA MSIMBAZI, MO AIDAI SIMBA BILIONI ZAKE.


MO anataka kulipwa pesa zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji
wa Simba tangu mwaka jana baada ya kubaini kuwa Simba imeingia mkataba
na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.
MO kawaandikia Simba ‘demand note’ kwa kua wamekiuka makubaliano yao
kwamba, atoe pesa kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na
ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja
viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini
viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.
Simba ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu
kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO
kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama
wakibaki na hasilimia 49.
Comments
Post a Comment