Mwigulu Nchemba: Bado Hatuna Sheria ya Kuthibiti Shisha
DODOMA: Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba bungeni leo amesema serikali bado haina
sheria ya kuthibiti matumizi ya kilevi aina ya shisha ila lipo agizo la
Waziri Mkuu la kupiga marufuku biashara hiyo na kutaka agizo hilo
lifuatwe na kila mtu.
Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati
akijibu swali bungeni kuhusu matumizi ya kilevi hicho cha shisha ambacho
bado katika baadhi ya maeneo kimeendelea kutumika na kuleta athari kwa
watumiaji.
“Ni
kweli serikali baada ya kuona matumizi ya kilevi cha Shisha yanaleta
athari kwa binadamu, serikali imeanza kuweka sheria za kuthibiti
matumizi ya shisha, usambazaji wa shisha na uagizaji wa kilevi hicho,
lakini wakati tunasubiri sheria hizo tunatambua kuwa lipo agizo la
Waziri Mkuu la kupiga marufuku matumizi ya kilevi cha shisha ambalo
utekelezaji wake ulianza mikoani kama Dar es Salaam, Mbeya, Iringa na
mikoa mingine imeendelea kuitikia. Kwa hiyo maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu
yanafanyiwa kazi bila kupunguza hata nukta” alisema Mwigulu Nchemba
Mbali na hilo Waziri Mwigulu alisema
anatambua wapo watu walipewa leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo
ya shisha lakini kwa kuwa serikali inajali masuala ya afya ya Watanzania
ndiyo maana wanatakakuja na sheria ili kuthibiti kilevi hicho ambacho
kina athari kwa watumiaji.
Comments
Post a Comment