Posts

Ndege mpya ya ATCL yapata hitilafu uwanja wa ndege Arusha

Image
Ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jana ilipata hitilafu katika uwanja wa ndege wa jijini Arusha hali iliyopelekea ndege hiyo kushindwa kuendelea na ratiba kama ilivyokuwa imepangwa. Taarifa kutoka katika uwanja wa ndege wa Arusha zinaeleza kuwa tairi moja ya ndege hiyo lilipata pancha ikiwa katika barabara ya kurukia ndege. Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa tairi moja ya ndege hiyo lilitoka nje ya barabara ya ndege kukimbilia wakati ndege hiyo ilipokuwa inatua uwanjani hapo hivyo ikakwama kwenye nyasi. Chanzo cha ndege hiyo kutoka nje ya barabara ya kukimbilia ndege kimeelezwa kuwa ni wembamba wa barabara hiyo kiasi kwamba rubani akikosea kidogo tu, basi ndege hutoka nje. Hadi sasa Shirika la Ndege la Tanzania halijatoa taarifa yoyote kuelezea tukio hilo.

Rais Magufuli Afanya Ziara ya Kushtukiza Gereza la Ukonga Dar

Image
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2016        Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Mkuu wa Magereza, John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2016 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016. Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John...

Pedeshee Ndama Kortini Kwa Kugushi Nyaraka na Kutakatisha Bil 1.77

Image
DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara wa jijini Dar, Ndama Shaaban Hussein almaarufu Pedeshee Ndama Mutoto ya Ng’ombe, aliyewahi kuwa mfadhili wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la utapeli wa dola za Kimarekani 540, 390 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 1.18. Ndama amesomewa mashtaka sita mbele ya Hakimu Victoria Nongwa na Mwendesha Mashtaka Leonard Msigwa akisaidiana na Christopher Challo kuwa, mnamo Februari 20, 2014 mkoani Dar, Ndama alitengeneza nyaraka feki, zikionesha kupata kibali cha kusafirisha sampuli za madini ya dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC). Shtaka la pili, tatu na nne pia yalikuwa ya kugushi nyaraka, ikiwemo iliyotoka Umoja wa Mataifa, iliyoisafisha kampuni yake ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Ltd kuwa imeruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu. Nyaraka hizo zililenga kuiaminisha Kampuni ya Trade TJL DTYL Lt...

Wananchi wa Cuba Watoa Heshima za Mwisho Kwa Mwili wa Rais Fidel Castro

Image
HAVANA, CUBA: Maelfu ya raia wa Cuba wanatoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi mwanamapinduzi Fidel Castro, aliyeaga dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 90. Ikiwa ni siku ya kwanza ya kipindi cha siku tisa za maombelezi rasmi ya kifo chake, misafara mirefu imeshuhudiwa katika uwanja wa Revolution Square katika Mji Mkuu Havana, sehemu ambayo waombolezaji wameweka picha ya kiongozi huyo akiwa ameshika bunduki. Siku za maombolezi zitakamilika baada ya majivu ya mwili wake kuzikwa siku ya Jumapili. Majivu ya Castro yalitazamiwa kuwasilishwa kwa umma katika uwanja wa Revolution Square lakini yamewekwa katika sehemu tofauti. ‘Roho ya Cuba’ Wananchi wengi wa Cuba walikuwa katika milolongo hata kabla ya alfajiri kuwadia ili kuhakikisha wako miongoni mwa watu wa kwanza kutoa heshima zao. Tania Jimenez, mwenye umri wa miaka 53, mwanahisabati, ameliambia shirika la habari la AP kwamba Fidel ni kila kitu kwao, na ni kiungo muhimu kwa nchi hiyo ...

Daktari Feki Afanya Upasuaji Wagonjwa 9 na Kufariki Mmoja, Apewa Ofa ya Kujiendeleza Kielimu

Image
KENYA: Kamati ya maswala ya afya nchini Kenya imependekeza daktari feki aliyekamatwa nchini humo aruhusiwa kujiendeleza na masomo ya udaktari badala ya kutumikia kifungo gerezani. Kauli hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa daktari huyo feki alifanikiwa kufanya upasuaji kwa wagojwa tisa ambao kati ya yao wanane walipona na mmoja ambae alikuwa mjamzito ndiye aliyepoteza maisha huku akifanikiwa kumuokoa mtoto aliyekuwemo tumboni mwa mjamzito huyo.

Njama 638 za Mauaji Alizoepuka Rais Fidel Castro

Image
Njama ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi? Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith. Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu. Mpenzi wa zamani wa Castro, Marita Lorenz alipewa dawa za sumu kumwekea katika kinywaji chake Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa, kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante. Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean. Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja...

Chanjo Dhidi ya Ukimwi Kuanza Kufanyiwa Majaribio Kesho Jumatano

Image
AFRIKA KUSINI: Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii. Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, Shirika la Habari la AP linasema. Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini. Washiriki hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35. Majaribio hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu “Ikitumiwa pamoja na silaha tulizo nazo sasa za kuzuia maambukizi, chanjo hiyo inaweza kuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Ukimwi,” Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Maradhi ya Kuambukizana na Mzio ya Marekani (NIAID) amesema kupitia taarifa. “Hata kama mafanikio yake yatakuwa ya kadiri, hilo linawez...

Kesi ya Mke wa Bilionea Msuya Yaahirishwa Tena

Image
DAR ES SALAAM: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Miriam Msuya aliyekuwa mke wa bilionea jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, kuhusu kufutiwa mashitaka ya madai ya kumuua wifi yake, Anethe Msuya yaliyotokea Mei 25, mwaka huu, Kigamboni, Dar. Miriam Msuya akitoka mahakamani baada ya kesi kuahirishwa. Uamuzi huo ungetolewa leo lakini kesi imeahirishwa kwa kuwa, Hakimu Mkazi Magreth Bankika anayesikiliza kesi hiyo, hakuwepo mahakamani. Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa, alisema kesi ilitajwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi lakini hakimu anayeisikiliza hakuwepo hivyo uamuzi utatolewa Desemba 8, mwaka huu. NA DENIS MTIMA/GPL

Machafuko Yanayoendelea Kwenye Kasri ya Mfalme Uganda, Mwandishi wa KTN Akamatwa

Image
Mwandishi wa habari wa runinga ya KTN ya nchini Kenya, Joy Doreen Biira amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa usalama nchini Uganda jana Jumapili usiku. Vyombo vya habari zinasema Bi Biira alikamatwa pamoja na wengine watano kwa tuhuma za kupiga picha na video kuhusu operesheni ya maafisa wa usalama katika kasri la mfalme wa Rwenzururu na kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii. Wanahabari na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wametoa wito kwa serikali kumwachilia huru. Hash Tag #FreeJoyDoreen (Mwachilie huru Doreen) kinavuma katika mtandao wa Twitter nchini Kenya. Wanajeshi na polisi walivamia kasri hilo la Mfalme Charles Wesley Mumbere Jumapili. Walinzi wake 46 waliuawa kwa mujibu wa polisi, na wengine 139 wakakamatwa. Mfalme huyo alikamatwa pia na kuzuiliwa makao makuu ya polisi ya wilaya ya Kasese kabla ya kuhamishiwa mjini Kampala. Gazeti la linalomilikiwa na Kampuni binafsi ya Monitor nchini humo linasema mfalme huyo anatarajiwa kukutana ...

Hatima ya Dhamana ya Godbless Lema Kujulikana Leo

Image
ARUSHA: Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo, anatarajia kujua hatima ya dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili. Lema anashikiliwa katika mahabusu ya Magereza ya Kisongo mjini Arusha. Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema. Amesema waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa. Katibu wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa. Lema alirudishwa mahabusu kutokana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kukataa kupokea ombi lake la kufanya marejeo ya uamuzi wa kunyimwa dhamana. Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mosha alisema uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi umeegemea kifungu cha Sheria cha Makosa ya Jinai CPA 148, hivyo kilimtaka mshtakiwa kukata rufaa siyo kuomba Mahakama hiyo kufanye reje...

Kiwanda cha Dangote Chasitisha Uzalishaji wa Saruji Mtwara Kutokana na Gharama Kuwa Juu

Image
MTWARA: Kiwanda cha Saruji cha Dangote huko Mtwara kimesitisha uzalishaji kutokana na gharama kuelemewa na gharama za uendeshaji hivyo kuwaacha watumiaji wake njia panda. Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Harpeet Duggal Walisema wapo na mazungumzo na serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo Mwezi uliopita mkurugenzi huyo alilalamika uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo alidai yapo chini ya kiwango na bei ghali. Pia alilalamikia shirika la maendeleo ya petroli TPDC kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alidai madai yao ya gharama kuwa juu ni ya uzushi. CREDIT: NIPASHE

Lady Jaydee Kaolewa na Rastaman?

Image
Staa wa Bongo Fleva, Lady Jaydee ‘Anaconda’  akiwa katika matembezi na Rastaman. Wakiwa katika mazungumzo matamatam katika Hoteli ya Serena visiwani Zanzibar. . Akimshangaa Rastaman. STAA wa Bongo Fleva, Lady Jaydee ‘Anaconda’  amenaswa akijiachia na Rastaman huyo sehemu mbalimbali wakiwa pamoja tokea  aachane na aliyekuwa  mume wake mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM,  Gardiner G Habash. Picha hizo zimeibua sitofahamu kwa mashabiki wake wakijiuliza kweli Rastaman huyo  ndiye shemeji yao? Mtandao huu ulijaribu kumtafuta meneja wa msanii huyo Seven kwa kumpigia simu hakupokea na tuliamua kumtumia meseji mpaka tunziweka picha hizi alikuwa ajatoa majibu.

Rais Magufuli Amuapisha Diwani Athumani Kuwa RAS Kagera

Image
    Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

RAIS MPYA WA TCCIA AKUTANA NA MWENYEKITI WA CEO ROUND TABLE

Image
 Ndibalema Mayanja akukutana na Mwenyekiti wa CEO Round Table Ali Mfuruki  ili kukuza mahusiano ya Taasisi hizi nyeti kwa maendeleo ya Biashara, Viwanda na Kilimo. Katika mkutano huo Rais Mayanja aliongozana na Makamu wa Rais wa TCCIA Viwanda Octavian Mshiu, Mkurugenzi Muganda na Mshauri wa TCCIA Imani Kajula.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JENERALI FAN CHANGLONG MAKAMU MWENYEKITI WA KAMISHENI KUU YA ULINZI YA JESHI LA UKOMBOZILA WATU WA CHINA (PLA)

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa...