Kesi ya Mke wa Bilionea Msuya Yaahirishwa Tena
DAR ES SALAAM: Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Miriam
Msuya aliyekuwa mke wa bilionea jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya,
kuhusu kufutiwa mashitaka ya madai ya kumuua wifi yake, Anethe Msuya
yaliyotokea Mei 25, mwaka huu, Kigamboni, Dar.
Uamuzi huo ungetolewa leo lakini kesi
imeahirishwa kwa kuwa, Hakimu Mkazi Magreth Bankika anayesikiliza kesi
hiyo, hakuwepo mahakamani.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu,
Victoria Nongwa, alisema kesi ilitajwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi
lakini hakimu anayeisikiliza hakuwepo hivyo uamuzi utatolewa Desemba 8,
mwaka huu.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
Post a Comment