Njama 638 za Mauaji Alizoepuka Rais Fidel Castro
Njama
ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana
sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi?
Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA
na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya
karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina
athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba
Wayne Smith.
Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba
alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa
miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.
Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa, kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.
Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa
utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza
kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.
Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja
ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi
ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika
Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza
boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa
mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.
Mipango yote hiyo ilitupiliwa mbali.
Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi
kuugundua,ripoti hiyo ilisema.
Mmoja ya wapenzi wa Castro wa zamani, Marita Lorenz alisajiliwa.
Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka
katika kinywaji cha Castro.Lakini Castro aligundua jaribio hilo na
anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.
”Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza
kuniua,”Bbi Lorenzo alisema Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na
gazeti la New York daily.
Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea
kuvuta sigara yake.”Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na
uhakika juu yangu.Alinikumbatia na tukafanya mapenzi”.
Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi
ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa
kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini
Panama.
Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.
Watu wanne ikiwemo mtoro mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.
Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya
Castro ambaye pia anajulikana ” The Beared” aonekana kama chombo cha
kukejeliwa badala ya kumuua.
Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu
vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo
kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.
Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya
Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu
ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.
Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New
York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia
wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina
kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.
”Nimevaa fulana ya kawaida”,alisema.
Miongo kadhaa awali mwaka 1975, tume ya
bunge la seneti nchini Marekani ilifichua maelezo ya njama nane dhidi ya
maisha ya Castro kwa kutumia vifaa ambavyo tume hiyo inasema
”vinachosha akili”.
Njama moja iliopangwa na ambayo karibu
ifaulu mara mbili ilikuwa ile ya kutuma dawa za sumu Cuba na kuwapeleka
watu kumuua kiongozi huyo.
Ulikuwa wakati kama huo ambapo rais
Kennedy, ambaye aliruhusu uvamizi wa kumuondoa madarakani rais Castro
mwaka 1961 aliuawa, ambapo ajenti wa CIA alikuwa anatoa kalamu yenye
sumu ilio na sindano kwa ajenti mmoja wa Cuba ili kumuua kiongozi huyo.
Comments
Post a Comment