Kiwanda cha Dangote Chasitisha Uzalishaji wa Saruji Mtwara Kutokana na Gharama Kuwa Juu

dangote-cement-complexMTWARA: Kiwanda cha Saruji cha Dangote huko Mtwara kimesitisha uzalishaji kutokana na gharama kuelemewa na gharama za uendeshaji hivyo kuwaacha watumiaji wake njia panda.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Harpeet Duggal
Walisema wapo na mazungumzo na serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo
pic+dangote
Mwezi uliopita mkurugenzi huyo alilalamika uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo alidai yapo chini ya kiwango na bei ghali.
Pia alilalamikia shirika la maendeleo ya petroli TPDC kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alidai madai yao ya gharama kuwa juu ni ya uzushi.
CREDIT: NIPASHE

Comments

Popular posts from this blog