Daktari Feki Afanya Upasuaji Wagonjwa 9 na Kufariki Mmoja, Apewa Ofa ya Kujiendeleza Kielimu
KENYA: Kamati ya maswala ya afya
nchini Kenya imependekeza daktari feki aliyekamatwa nchini humo
aruhusiwa kujiendeleza na masomo ya udaktari badala ya kutumikia kifungo
gerezani.
Kauli hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa daktari huyo feki
alifanikiwa kufanya upasuaji kwa wagojwa tisa ambao kati ya yao wanane
walipona na mmoja ambae alikuwa mjamzito ndiye aliyepoteza maisha huku
akifanikiwa kumuokoa mtoto aliyekuwemo tumboni mwa mjamzito huyo.
Comments
Post a Comment