Posts

Mbunge aangua kilio msibani

Image
Mbunge huyo akilia. Stori: Imelda Mtema, UWAZI D AR ES SALAAM: Ukimwona mtu mzima analia, ujue kuna jambo! Mbunge wa Jimbo la Tarime (CCM) kwa miaka mitano (2010-2015), Nyambari Chacha Mariba Nyangwine (40), amejikuta akimwaga machozi kwenye misa ya kuuombea mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni yake ya kuchapa vitabu ya Nyambari Nyangwine Publishers, marehemu Edwin Semzaba (pichani). Tukio hilo lilijiri hivi karibuni kwenye Kanisa Katoliki  Mlimani jijini Dar ambako mwili huo ulikuwa ukifanyiwa ibada na kuagwa. Wakati Semzaba akikutwa na mauti, Nyambari alikuwa kwenye safari ya kibiashara nchini Brazil ambapo baada ya kupokea taarifa hizo alikatisha shughuli zake nchini humo na kurejea Tanzania kwa mazishi.   Akizungumza na Uwazi jijini Dar juzi, Nyambari alisema alilia kwa sababu marehemu alikuwa msaada mkubwa kwake katika biashara ya vitabu. “Mimi nje ya ubunge ni mchapishaji mkubwa wa vitabu. Marehemu alikuwa mkurugenzi kwenye kampuni ya...

TWIGA ALIBINO APATIKANA TANZANIA,AWA GUMZO ,ASHANGAZA WENGI

Image
Wataalamu wasema kuna hatari ya kuwindwa na majangilihivyo wanatakiwa kupewa ulinzi wa kutosha      Mwanasayansi Dk Derek Lee amegundua twiga albino kwenye hifadhi ya mbuga ya Tarangire iliyopo katika Mkoa wa Arusha nchini Tanzania. Mtafiti huyo Dk Derek Lee, alipiga picha mbalimbali zikiwa zinamwonyesha mnyama huyo akiwa katika kundi kubwa la twiga, huku akiwa na rangi ya kipekee ikilinganishwa na twiga wengine duniani. Dk Lee, alimgundua twiga huyo wakati akifanya utafiti kwenye mbuga hiyo na nyingine za wanyama za barani Afrika, Taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari nchini Uingereza kupitia gazeti la Dailymail zimeeleza kuwa, twiga huyo adimu kupatikana duniani iwapo atahifadhiwa atakuwa kivutio cha pekee katika mbuga hiyo. Twiga huyo anayejulikana kitaalamu kwa jina la ‘Omo’ likimaanishwa twiga mweupe/mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino’, alionekana akizunguka katika mb...

Mume amuua mke mjamzito!

Image
Marehemu Clara Justin Munishi enzi za uhai wake. Stori: Makongoro Oging’, UWAZI D AR ES SALAAM: Dunia katili! Clara Justin Munishi (30), mkazi wa Keko Mwanga, Temeke jijini Dar amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na kujeruhiwa vibaya na mumewe, Novatus Peter Kabero. Tukio hilo la kikatili, lilitokea usiku wa saa tano, Januari 13, 2016 nyumbani kwa wanandoa hao ambapo kwa mujibu wa majirani, mwanamke huyo alisikika akilia na kuomba msaada kwa muda mrefu kutokana na kushushiwa kipigo kikali na mumewe. Mume wa marehemu   Novatus Peter Kabero. “Unajua hawa ilikuwa kama kawaida yao kugombana, mara kwa mara mwanaume alikuwa akimpiga sana mkewe hasa nyakati za usiku. Sasa siku hiyo hata tuliposikia Analia na kuomba msaada, tulijua ni kama kawaida yao, kumbe mwenzetu alikuwa anauawa,” alisema mwanamke mmoja anayeishi jirani na eneo la tukio, aliyekataa kujitambulisha jina lake. Habari zaidi kutoka kwa vyanzo vyetu, zinaeleza kuwa baada ya kuzidiwa na kipigo,...

Simbachawene Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Simbachawene. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Simbachawene amemvua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Augustino Kalinga kufuatia kuruhusu ofisi yake kuwachangisha wazazi michango ambayo serikali imezuia katika kutoa elimu ya msingi bila malipo. Mh. Simbachawene alifikia uamuzi huo jana mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya kugundua kuwa manispaa ya Dodoma imesambaza barua kwa walimu wakuu wa shule za msingi ambazo zimeagiza kuwatoza wazazi michango ya maji, umeme na mlinzi ambayo imekatazwa na serikali. Amesema kuwa Bw. Kalinga amevuliwa madaraka yake baada ya kubainika kuwa ameshindwa kuwasimamia watumishi walio chini yake hadi kusababisha kuandika barua na kusambaza kwa walimu wakuu wa shule za msingi katika manispaa ya Dodoma amb...

NYUMBA YA MCHUNGAJI RWAKATARE YASABABISHA WAZIRI JANUARY KUCHUKUA HATUA HIZI KALI KWA MAOFISA HAWA

Image
SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi. Akizungumza  jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani. Maofisa waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi. Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia ki...

Wema Sepetu na Idriss Sultan Wavujisha Picha Wakiwa Kitandani Kama zile za Watuache Tulale..Mashabiki Walalamika

Image
Picha za Wema Sepetu na Idriss Wakiwa kitandani asubuhi ya leo zimesambaa katika mitandao ikiwa ni siku moja tu baada ya Idriss kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi na kuwa wanakaribia kupata mtoto... Mashabiki wa couple hiyo inayoongelewa zaidi kwa sasa wametoa maoni yako katika picha hizo, hapa nimekuwekea baadhi ya maoni;  tamia_ismail @zara_elia u u gat the point,l lov ths lady ila apo tu ndo anaponiudhi ...she like to expose evrythin i wsh she cn lern to keep othr things fr herself wala asingekua midomon mwa watu..anyway evry one has got a weaknes sy_salum_y_madai  Wewe idrus chaliloo ukija machimboni R chugga lazima tukuwekechini...maan kweli... Ustaa wa gafla unakuzingua maan wakati tumetoka mbali Manzi yako umemwacha bonge lakisu unaenda Pambana na makonkodi maan... Dah unazingua maan  team.watafutaji  Kila mwanaume anamtimia wema kwa manufaa yake na kujipatia umaarufu pcolour543  Tushazoea huyo dada na hzo picha.. Sio a...

Mrembo wa UDSM aliyedaiwa kuwa Msukule uliokutwa shimoni anena kwa uchungu

Image
Picha zinazomuonesha mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya kutisha zimetumiwa kufanya upotoshaji kwa kumzushia msichana mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha iliyounganishwa ikionesha taswira ya msichana huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakidai kuwa hapo ni kabla zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema na kusababisha usumbufu kwa mrembo huyo. Msichana huyo ambaye anatumia jina la Ms.Adelaide kwenye Instagram amekanusha vikali taarifa hizo huku akieleza kwa uchungu jinsi ambavyo ameathiriwa na uzushi huo. “ NAJUA WENGI MTAKUA MMEKUTANA NA HIZI HABARI..SIJAJUA NANI ALIEANZISHA HII MADA NA SIJUI IMEANZIA KWA NANI. MIMI NI MZIMA NA SIO MSUKULE JAMANI NINA WAZAZI WOTE WAWILI WAPO HAI NA WAMEUMIZWA SANA NA HIKI KITENDO, MY FAMILY MEMBERS WAMEUMIA MNOOO KUPITA KIASI, LICHA YA HIYO MIMI BADO NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, WANAFUNZI WENZANGU WENYE MAPENZI NA MIMI WANAUMIA...

Uchaguzi Zanzibar Wazidi Kukosolewa..Mwanasiasa Mwingine Mkongwe Atoa ya Moyoni

Image
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo. Amesema jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo, amesema kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema. Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana.  Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi  wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza  wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao. “Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutw...

Wema Sepetu Could Now Be Having a Baby with BBA Winner Idris Sultan

Image
After some ups and downs with Diamond Platnumz and Ommy Dimpoz and scuffles with Zari Hassan over Diamond, Wema’s heart has finally found a resting place. And the lucky man is none other than Idris Sultan. Idris took to social media to declare his undying love for the former Miss Tanzania and even hinted that they could be expecting a baby: “ Me and You are not the ordinary. I sleep, eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama   "Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike"   au ukiingia jikoni kwangu and take over my house with good food. The way you look at other women wakinisogelea, how you always know when i need a kiss or a tight hug. The way you force me kuangalia Disney channel, how you wake up e...

DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KAZI RASMI MACHI MOSI.

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa nne kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Katibu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.    Msimamizi na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo, akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa kwanza kulia)  sehemu ya kipande cha km 1.5 kilichopo upande wa Kigamboni kwa ajili ya upanuzi wa daraja hilo.   Mwonekano wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.   Lango la kuingilia daraja la Kigamboni li...

DK.MAGUFULI AAGIZA MABALOZI WALIOMALIZA MUDA WAO WAREJESHWE NCHINI MARA MOJA

Image
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli   kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili  2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa 2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki. 2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni: 2.2.1 Bi Batilda Salha BURIAN...

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUWA MAHADHI JUMA MAALIM KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KUWAIT

Image
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam. Na Eleuteri Mangi-MAELEZO  Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki. Vile vile Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha na kuwataka Mabalozi hao kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliyechini yao leo hii. Mabalozi hao ni Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan, Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia. Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Rais pia amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan Kallaghe ambaye anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrik...

MATUKIO KUTOKA BUNGENI -MJINI DODOMA JANUARI 25, 2016.

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki akiteta na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji bungeni mjini Dodoma Januari 25, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majalaliwa  akisalimiana na Mbunge wa  Nkansi Ally Kessy kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majalaliwa  akisalimiana na Mbunge wa  Mbozi Magharibi,David Silinde kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016. Katikati ni Mbunge wa Nkansi, Ally Kessy. Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Januari 25, 2016. Katikati ni mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee kutoka jimbo la Chemba  Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Januari 25,2016.  Kushoto kwake ni Mbunge wa Chemba Juma Nkamia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

What Your Sleeping Position Says About Your Relationship

Image
Do you know that your sleeping position can tell a lot about your relationship? The thing is, in your sleep you can’t imitate or hide your emotions. Your subconscious feelings and attitude are on the surface when you sleep. That’s why you should pay attention to your and your partner’s sleeping positions to analyze your relationship. Sex expert Tracy Cox thinks that the closer you and your partner sleep, the stronger your relationship is. Here are several positions and their real meaning. It’s time to find out do you and your beloved one realy match! “Touching” Positions No matter what position you choose – you touch while sleeping. If so, that means you are committed lovers. You care about each other and keep your connection 24/7. There can be several variations of the position: If your partner’s arm is hugging you that means he is imperious, strives to dominate and in a way, control you. If his hand is between your hips or under your arm – that means his desire t...

Usajili Ulaya Ulimwengu akamilisha mazungumzo na St.Etienne.

Image
Wakati Mbwana Samata akiwekewa vikwazo kuondoka TP Mazembe, hali ni tofauti kwa Thomas Ulimwengu, ambaye yeye mambo yamemnyookea. Mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu ameshakamilisha mazungumzo na Klabu ya Saint Etienne ya Ufaransa na kinachosubiriwa ni yeye kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo. Ulimwengu amesema kabla ya dirisha dogo la usajili barani Ulaya kufungwa mwezi ujao tayari atakuwa ameshatua Ufaransa kuanza maisha mapya ya kusakata kandanda barani ulaya. Ulimwengu ameileza StarTv kuwa mmiliki wa TP Mazembe, Mose Katumbi amebariki kuondoka kwake. Ulimwengu ameweka bayana kuwa amechagua kwenda Saint Etienne kwa kuwa klabu hiyo inamsajili moja kwa moja bila kufanya majaribio. Klabu ya Saint Etienne inayoshiriki ligi kuu nchini ufaransa kwa sasa inashika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa nyuma ya point 4 na timu ya Monaco inayoshika nafasi ya pili na point 34. Hii ni kusema kwamba kama dili la Ulimwengu litakamilika na S...

BREAKING NEWS : BASI LA BM LAPATA AJALI ENEO LA MIKESE MOROGORO,LAUWA WAWILI

Image
Basi la BM lenye namba za usajili T619 BOX baada ya kugongana na lori leo eneo la Lubungo Mikese, barabara ya Morogoro-Dar es Salaam. WATU wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baàda ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.         ITV imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kushudia majeruhi wa basi hilo la kampuni ya BM wakiletwa kwa magari binafsi na basi jingine la kampuni hiyo, wakionekana kujeruhiwa zaidi maeneo ya kichwani, usoni na miguuni, ambapo mwandishi alilazimika kuweka kalamu pembeni na kusaidiana na wananchi wengine kuwabeba majeruhi na kuwaingiza kwa madaktari kupata huduma ya kwanza,huku vitanda vya kuwabebea vikionekana ...