NYUMBA YA MCHUNGAJI RWAKATARE YASABABISHA WAZIRI JANUARY KUCHUKUA HATUA HIZI KALI KWA MAOFISA HAWA
SAKATA
la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao
ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe
mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi.
Akizungumza
jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha
mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya
uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Maofisa
waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa
Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili
Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi.
Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha
kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
Pamoja
na maofisa hao, pia Mwanasheria Mnyele, anayetuhumiwa kuingia mkataba
na Mchungaji Getrude Rwakatare wa kuondoa kesi mahakamani kwa niaba ya
NEMC bila kuijulisha ofisi, naye anachunguzwa na taasisi hiyo ya rushwa.
Mama
Rwakatare kwa sasa ana kesi mahakamani dhidi ya baraza hilo ya kupinga
kubomolewa kwa nyumba yake, inayodaiwa kujengwa mahali pasiporuhusiwa.
Kiwanda
hicho cha minofu ya Punda cha China, kilianza kazi hiyo rasmi mwaka
2012 huko Dodoma ambapo pamoja na kuchinja, pia huuza nyama hiyo nje ya
nchi, hususan China.
Kiwanda
hicho kilipatiwa vibali vyote, ikiwemo cha Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa
Uwekezaji nchini (EPZA) na cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha
kuchinjia.
Pia, kilikuwa na vibali vingine vya Manispaa. Hata hivyo, hakikuwa na kibali cha masuala ya mazingira kutoka NEMC.
Katika
ukaguzi uliofanywa siku za nyuma na Baraza hilo, ilibainika kuwa
kiwanda hicho hakina kibali hicho cha mazingira, lakini pia kilikuwa
kikilalamikiwa na wananchi wanaokizunguka kutokana na kutofuata taratibu
za utunzaji wa mazingira.
NEMC
ilibaini kuwa kiwanda hicho, hakikuwa na mfumo wa majitaka, lakini pia
kilikuwa kikichoma mabaki yanayotumika kuchinjia ndani ya kiwanda hicho
na moshi wake kusambaa maeneo yanayokizunguka.
Kutokana na makosa hayo, baraza hilo lilikifungia kiwanda hicho kama adhabu na kukilipisha faini ya Sh milioni 240.
Juzi
Waziri January pamoja na kuwasimamisha maofisa hao watatu kwa kukiuka
miiko yao ya kazi, pia aliagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Mhandisi
Bonaventura Baya, apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma za
udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa baraza hilo, hivyo kusababisha
malalamiko mengi kuhusu utendaji wa baraza hilo.
Comments
Post a Comment