Uchaguzi Zanzibar Wazidi Kukosolewa..Mwanasiasa Mwingine Mkongwe Atoa ya Moyoni
Waziri
Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo.
Amesema
jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo, amesema kinachotakiwa
hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta
suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo
si jema katika sura ya kimataifa,” alisema.
Mwanadiplomasia
huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha
Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka
jana. Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi wa Zanzibar ni jambo
lililowashangaza wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na
utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao.
“Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika
nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya
uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutwa
kumewashangaza wengi na bado suala hili halieleweki. “Pia hili jambo
sidhani kama ni la mtu mmoja…sidhani kama ni la Jecha peke yake. Huu si
mustakabali mzuri kabisa, Zanzibar ni nchi ndogo, lakini ina historia
kubwa kisiasa hivyo juhudi za pamoja zifanyike kutatua mgogoro huu kwa
matakwa ya Watanzania kwa ujumla.
Comments
Post a Comment