DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KAZI RASMI MACHI MOSI.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng.
Joseph Nyamhanga (wa nne kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi na
Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa
Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto)
wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Katibu huyo kukagua
maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Msimamizi
na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko
wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo, akimuonesha Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng.
Joseph Nyamhanga (wa kwanza kulia) sehemu ya kipande cha km 1.5
kilichopo upande wa Kigamboni kwa ajili ya upanuzi wa daraja hilo.
Mwonekano
wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja
hilo linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.
Lango
la kuingilia daraja la Kigamboni linavyoonekana, pembeni ni ofisi za
huduma mbalimbali zitakazokuwa zinatolewa darajani hapo.
Sehemu ya juu ya daraja la Kigamboni, likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng.
Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni litaanza kutumika kuanzia
Machi mwaka huu.
Akizungumza
mara baada ya kukagua hatua za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga
amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha hatua ya ujenzi iliyobaki
inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi mwanzoni mwa mwezi
Machi.
“Hakikisheni
Machi mosi magari yaanze kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo
kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu
wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”, amesema
Eng. Nyamhanga.
Eng.
Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuunganisha
daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi hadi Chalinze ili
kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Amemtaka
meneja wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha anatafuta Wakala makini
atakayesimamia na kuendesha mradi huo.
Daraja
la Kigamboni lenye urefu wa mita 680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi zaidi ya miaka 100 na
kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56 zinazokubalika katika nchi
za jumuiya ya madola.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Comments
Post a Comment