RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUWA MAHADHI JUMA MAALIM KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KUWAIT
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mhe.
Rais Dkt. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma
Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kufuatia uamuzi wa Serikali
kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.Vile
vile Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na
Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja
Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha na kuwataka Mabalozi hao
kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliyechini yao leo hii.Mabalozi hao ni Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan, Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia.
Kwa
mujibu wa Balozi Sefue, Rais pia amemrejesha nyumbani Balozi wa
Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan Kallaghe ambaye
anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa
Kikanda na Kimataifa ambapo atakapopangiwa kazi nyingine.
Balozi
Sefue alisema kuwa hadi sasa vituo vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni
London nchini Uingereza kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A.
Kallaghe, Brussels nchini Ubelgiji kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt.
Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa Mbunge, Rome nchini Italia, kufuatia
kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex Msekela na Tokyo nchini Japan,
kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda Buriani.
Vituo
vingine vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni Kuala Lumpar nchini Malaysia,
kufuatia aliyekuwa Balozi Dkt. Aziz Ponray Mlima kuteuliwa kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa
Kikanda na Kimataifa na Brasilia nchini Brazil, kufuatia kustaafu kwa
aliyekuwa Balozi, Bwana Francis Malambugi.
Wakati huo Balozi Sefue alisema kuwa Rais ametengua uteuzi wa Mhandisi Madeni Juma Kipande kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.
Comments
Post a Comment