Mbunge aangua kilio msibani



mbunge (1)-001
Mbunge huyo akilia.
Stori: Imelda Mtema, UWAZI
DAR ES SALAAM: Ukimwona mtu mzima analia, ujue kuna jambo! Mbunge wa Jimbo la Tarime (CCM) kwa miaka mitano (2010-2015), Nyambari Chacha Mariba Nyangwine (40), amejikuta akimwaga machozi kwenye misa ya kuuombea mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni yake ya kuchapa vitabu ya Nyambari Nyangwine Publishers, marehemu Edwin Semzaba (pichani).
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni kwenye Kanisa Katoliki  Mlimani jijini Dar ambako mwili huo ulikuwa ukifanyiwa ibada na kuagwa.
Wakati Semzaba akikutwa na mauti, Nyambari alikuwa kwenye safari ya kibiashara nchini Brazil ambapo baada ya kupokea taarifa hizo alikatisha shughuli zake nchini humo na kurejea Tanzania kwa mazishi.
mbunge (5)-001 
Akizungumza na Uwazi jijini Dar juzi, Nyambari alisema alilia kwa sababu marehemu alikuwa msaada mkubwa kwake katika biashara ya vitabu.
“Mimi nje ya ubunge ni mchapishaji mkubwa wa vitabu. Marehemu alikuwa mkurugenzi kwenye kampuni yangu. Sasa kusikia ameaga dunia, kwa kweli niliumia sana.
“Nilipokuwa nauaga mwili kwake, hali haikuwa nzuri. Nilijikuta machozi yakitoka yenyewe,” alisema Nyambari.
Semzaba ambaye pia alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (Uwaita) alifariki dunia Januari 16, mwaka huu kwa matatizo ya presha. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Atakumbukwa zaidi kwa kitabu chake cha Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe kilichompatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog