DK.MAGUFULI AAGIZA MABALOZI WALIOMALIZA MUDA WAO WAREJESHWE NCHINI MARA MOJA
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili
2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
2.2 Rais
ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa
Kanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao
mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa
Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:
2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan
2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.
2.3 Rais
amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana
Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki
na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.
2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:
2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE
2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA kuchaguliwa kuwa Mbunge.
2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.
2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI
2.4.5
Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray
MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika
Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.
Comments
Post a Comment