Simbachawene Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Simbachawene.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Simbachawene
amemvua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Bw.
Augustino Kalinga kufuatia kuruhusu ofisi yake kuwachangisha wazazi
michango ambayo serikali imezuia katika kutoa elimu ya msingi bila
malipo.
Mh. Simbachawene alifikia uamuzi huo
jana mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua
zilizochukuliwa na serikali baada ya kugundua kuwa manispaa ya Dodoma
imesambaza barua kwa walimu wakuu wa shule za msingi ambazo zimeagiza
kuwatoza wazazi michango ya maji, umeme na mlinzi ambayo imekatazwa na
serikali.
Amesema kuwa Bw. Kalinga amevuliwa
madaraka yake baada ya kubainika kuwa ameshindwa kuwasimamia watumishi
walio chini yake hadi kusababisha kuandika barua na kusambaza kwa walimu
wakuu wa shule za msingi katika manispaa ya Dodoma ambayo inatofautiana
na maelezo ya serikali yaliyopo kwenye mwongozo.
Aidha, amebainisha kuwa katika
mwongozo wa elimu ya msingi uliotolewa na serikali unafafanua majukumu
ya wazazi na walezi ambayo wanatakiwa kuyafanya kuwa ni pamoja na sare
za shule, vifaa vya michezo na vya kujifunzia pamoja na matibabu na
chakula.
Comments
Post a Comment